NA FARIDA MANGUBE.

Katika kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri mahala pa kazi Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kimewakutanisha wafanyakazi wake kwenye hafla ya Iftar iliyonyika katika ukumbi wa Freedom Square uliopo Kampasi ya Solomon Mahlangu.


Akizungumza kwenye hafla hiyo Prof. Raphael Chibunda amesema Chuo kimekuwa na desturi ya kufuturu pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.


“Mara zote tumekuwa tukifanyia hafla hii katika Kampasi ya Edward Moringe, mwaka huu tumeamua kuandaa hafla hii Kampasi hii ya Solomon Mahlangu ni washukuru Waislamu na wote mliohudhuria katika Iftar ya leo mmetuheshimisha sana kwa kuacha shughuli zenu nyingi na kujumuika nasi.” Alisema Prof. Chibunda.


Aidha amewataka wafanyakazi kuendelea kuishi kwa umoja na upendo kama wanavyoishi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na kwamba mwezi utakapomalizika kuendeleza yote yaliyo mema ikiwa ni pamoja na kwenye maeneo yao ya kazi.


Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mussa Ally Mussa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Bi. Fatma Mwassa amesema ni vyema Taasisi kukutanisha wafanyakazi ili kudumisha umoja baina yao.


Share To:

Post A Comment: