Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kimetoa msaada wa chakula na vitu mbalimbali katika kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Vitu vilivyotolewa ni pamoja na Mchele, Maharage, Mafuta ya kupikia, Mafuta ya kujipaka, Sukari,unga wa sembe, Sabuni za kufulia, Miswaki na mbuzi wawili kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa mwaka huu 2023.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Bwana Michael Henerco ameiasa jamii, viongozi mbalimbali na wadau kwa ujumla kuwa na moyo wa majitoleo kwa watu wenye uhitaji ili kuendelea kupata baraka za mwenyezi Mungu.

“Tunapokuja hapa tutambue kuwa ni wajibu watu na kwamba mambo tunayoyafanya hapa tutambue kwamba tunatakikana kuyafanya kwahiyo kuja hapa ni tone kwa maana ya kwamba ni kupata chachu ya kukumbuka kuendelea kuwakumbuka wazee popote unapokutana nao, panga tu katika familia yako kufanya mambo ya kiibada kama haya siyo lazima sana uje kwenye kituo kama tulivyofanya  sisi”.

“Wafundishe watoto wako kufanya matukio ya kiibada kwa wazee na watu wengine wasiojiweza wakikutana nao kwa sababu utakapofika muda na wewe unahitaji kupata msaada kama watoto wako hukuwafundisha usitegemee watakusaidia, kwahiyo niendelee kuwasisitiza kuwa moyo huu tuendelee kuwa nao na tuufanye kwa uthabiti sana nasisi chuo cha Sayansi za Afya kolandoto tumeanza na tunaendelea wazee pamoja na watu wengine wenye uhitaji”.amesema Kaimu mkuu wa chuo bwana Henerco

Kwa upande wake Afisa Mfawidi wa kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto Bi. Sophia Kang’ombe ameshukuru kwa msaada huo na kubainisha kuwa kituo hicho bado kinauhitaji ambapo amewaomba viongozi katika taasisi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuguswa kwa majitoleo ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto zilizopo.

“Nakushukuru sana kaimu mkuu wa chuo pamoja na timu nzima yako ya watumishi kwa kuweza kuguswa kutuletea zawadi ya Pasaka kwa wazee wetu kwa kweli Mungu awabariki kwa jambo hili nawaomba tuendelee kushirikiana siku zote”.

“Na nitoe wito kwa wadau wengine wa nadani na nje ya Mkoa wa Shinyanga tunamahitaji mengine ambayo bado wazee wetu wanahitaji tofauti na chakula tunahitaji kupata jengo lingine kubwa ili wazee wetu waweze kupata nafasi ya kutosha kukaa kila mmoja kwenye chumba chake bado tunawaomba wadau popote pale walipo karibuni muweze kuunga juhudi za serikali katika kuwatunza wazee”.amesema Bi. Sophia Kang’ombe

Nao baadhi ya wazee hao wameshukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kupunguza  changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.

 

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Bwana Michael Henerco akizungumza katika hafla hiyo.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Bwana Michael Henerco akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Mfawidi wa kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto Bi. Sophia Kang’ombe akizungumza katika hafla hiyo.

 

Hafla ya kukabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali ikiendelea leo April 5,2023 katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Mkoani Shinyanga 

 Mwalimu mkufunzi idara ya uuguzi Kolandoto College of Health Science (Afisa muuguzi) Elikana Wallace upande wa kulia akitoa elimu juu ya ugonjwa wa Kisukari.

Wazee na wasiojiweza kituo cha Kolandoto wakiendelea kupima juu ya ugonjwa wa kisukari
Zoezi la vipimo juu ya ugonjwa wa kisukari likiendelea katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto likiendelea katika hafla ya kukabidhi msaada.
Share To:

Misalaba

Post A Comment: