Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati akifungua semina  ya siku mbili ya Wahariri wa vyombo vya habari Aprili 5, 2023, iliyoandaliwa na MSD ambayo inafanyika  mkoani Dodoma.

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

BOHARI ya Dawa (MSD) inatarajia kujenga maghala matano kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kagera, Dodoma na Mtwara ili kuboresha huduma za utendaji wa kazi zao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika semina iliyoandaliwa na MSD ambayo inafanyika  mkoani Dodoma.

“Maghala haya yatasaidia kuboresha huduma zetu za kusambaza dawa na vifaa tiba kwa wananchi hasa katika mikoa ambayo ina watu wengi kama Mwanza, Dar es Salam na Kagera” alisema Tukai.

Tukai alitaja mikoa ambayo yatajengwa maghala hao kuwa ni Kagera, Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam na Mtwara.

Akizungumzia maboresho ya utendaji kazi wa MSD alisema wameanzisha mfumo wa kufanya kazi kwa njia ya mtandao na kuachana na ule wa kutumia makaratasi jambo ambalo litaongeza ufanisi wa kazi na kila jambo kuwa wazi.

“Tumeanza kufanya majaribio kwa kufanya kazi kwa njia ya mtandao tena kwa uwazi ambapo kila mtumishi wetu atakachokuwa akikifanya kitaonekana jambo ambalo litasaidia kuondoa changamoto na urasimu kazini” alisema Tukai.

Alisema hakuna sababu ya kuficha taarifa za umma kwani kila mtu anatakiwa kuziona na kupitia mfumo huo wa njia ya mtandao wataweza kuwabaini wafanyakazi wao pale watakapokuwa wakifanya kazi chini ya kiwango.

Aidha Tukai alisema MSD inatarajia kufungua Kampuni Tanzu ambayo itasimamia viwanda vya uzalishaji ambavyo vitaendeshwa na MSD na wadau wengine.

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati akifungua semina hiyo alisema Serikali imetoa fedha Sh.Bilioni 200 kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba lakini fedha ambazo zimepokelewa na MSD ni Sh. Bilioni 145.9.

Aidha Msasi aliwataka wahariri wa vyombo vya habari  kuwasiliana na wahusika kabla ya kutoa habari ambazo zinaweza kuleta taharuki kwa wananchi hasa zile zinazohusisha afya za watu.

Msasi alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai kwa  kuboresha mambo kadhaa ya MSD kwa muda wa miaka miwili ya ufanyaji kazi wake tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.

Msemaji wa Serikali, Geryson Msigwa akizungumza katikasemina hiyo.
Meneja Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hipoliti Lello akizungumza kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Mavere Tukai, akizungumza kwenye semina hiyo
Mkurugenzi, Uendeshaji Huduma wa Mamlaka ya Ukaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Chrispin Severe akizungumza kwenye semina hiyo.
Afisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka, akizungumza kwenye semina hiyo.
Taswira ya semina hiyo
Wahariri wakiwa kwenye semina hiyo.
Wahariri wakiwa kwenye semona hiyo
Semina ikiendelea

Semina ikiendelea
Menejimenti ya MSD wakijitambulisha.
Semina ikiendelea

Semina ikiendelea

 Wahariri wakiwa kwenye semina hiyo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: