Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mchungaji mstaafu wa Kanisa la AICT Randichi Nchini Kenya, Johana Wafula amewakumbusha wakristo kuendelea kusherehekea siku kuu ya Pasaka kwa kumpa Yesu nafasi ya kukaa moyoni katika maisha ya kila siku.

Ameyasema hayo wakati akihubiri kwenye Ibada ya mkutano wa Pasaka katika Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga ambapo mkutano huo umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi na nje ta Mkoa wa Shinyanga ikiwemo kwaya ya AICT Bariadi kutoka Mkoani Simiyu.

Mchungaji Wafula amesema ni muhimu kwa kila mkristo kutambua kuwa Yesu ndiye ufufuo na uzima wa milele hivyo amesisitiza wakristo kusimama imara ikiwa ni pamoja na kutenda matendo mema yanayompendeza mwenyezi Mungu ili kuendelea kupata baraka katika maisha ya kuishi hapa Duniani.

Amesema wakristo wanapaswa kuendelea kumtumaini Yesu katika shida na raka kwa kumpa nafasi kukaa moyoni ili kuepukana na mambo yakidunia yasiyofaa.

Wakristo Duniani  leo Jumapili (Aprili 9, 2023), wamejumuika kusherehekea siku kuu ya Pasaka ikizingatiwa kuwa siku hii ni ya ufufuo wa Yesu Kristo, ambaye alisulubishwa na askari wapanda farasi wa Kirumi na kufa siku ya Ijumaa Kuu.

Mchungaji mstaafu wa Kanisa la AICT Randichi Nchini Kenya, Johana Wafula akihubiri kwenye mkutano wa Pasaka katika Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

Mchungaji Charles Lugembe wa Kanisa la AICT Kambarage akiongoza ibada hiyo ya Mkutano wa Pasaka uliofanyika kwenye uwanja wa Kanisa hilo mjini Shinyanga.

Kwaya ya AICT Bariadi ikiimba kwenye mkutano wa Pasaka katika Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.











Share To:

Misalaba

Post A Comment: