mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi kiasi cha shilingi 850, 000 kwa uongozi wa watu walemavu


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred Daud Yassinamewakabidhiviongozi wa Chama cha Riadha cha watu wenye ulemavu Mkoani Iringa kiasi cha shilingi 850, 000/=


Comred Yassin ametoa fedha hiyo ili kufanikisha safari yao ya kwenda Dar es Salaam kwenye mashindano ya watu wenye ulemavu.


Kiongozi huyo wa CCM Mkoa wa Iringa amekabidhi kiasi hicho kutokana na maombi aliyopokea kutoka kwa  viongozi wa chama hicho.


"Nafurahi kwamba mliniandikia kuniomba mchango wa tshs 850,000/=  zimepatikana zote kama mlivyoniomba, ombi langu kwenu mkazitumie kama ilivyokusudiwa na hapana shaka mtarudi na ushindi," amesema Mwenyekiti Yassin


kwa upande wao vongozi hao wa Chama Cha riadha cha watu wenye ulemavu mkoani Iringa, wamemshukuru Comred Yassin, kwa moyo wake wa upendo kwao.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: