Na John Walter-Babati


Wananchi wa Kijiji cha Tsamas Kata ya Qash, wilayani Babati wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo kwa kutekeleza ahadi yake ya kufungua barabara ya Tsamas-Galapo huku wakiipa jina la Mbunge huyo.

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi kata ya Qash Iddy Matata amesema tangu kijiji hicho kiundwe mwaka 1974 hakikuwahi kuwa na bara bara Mpaka Mwaka 2023 baada ya Mbunge Daniel Sillo kushughulikia.

Amesema barabara hiyo ilikuwa haipitiki, na sasa inapitika jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa kijiji chao maarufu kwa kilimo cha mazao mbalimbali.

Aidha wameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kijiji chao.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Babati Mhandisi Aloyce Nombo amesema wataendelea kurekebisha bara bara zote katika wilaya na kuzifungua mpya.

Pamoja na hayo Wananchi hao, Viongozi wa dini mbalimbali walifanya maombi maalum kwa ajili Mbunge huyo.
Share To:

Post A Comment: