Na, Elizabeth Paulo, Dodoma

Wizara ya Nishati ikishirikiana na Mdari wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) inatekeleza Mradi wa Utekelezaji wa Matumizi Bora ya Nishati nchini kwa ufadhili wa Jumuiya ya umoja wa ulaya.


Mradi huu unafadhiliwa kwa garama za Uro millioni 8 kutoka jumuiya ya Ulaya huku UNDP ambao ni washirika katika utekelezaji wa Mradi wamefadhili Uro millioni 1 kufikisha jumla ya Uro millioni 9 sawa na shilingi za kitanzania za utekelezaji wa mradi huo.

Hayo yameelezwa leo machi 22,2023 Jijini Dodoma na Elimian Nyanda kutoka Wizara ya Nishati ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Utekelezaji wa Matumizi Bora ya Nishati wakati wa Kikao cha wadau wa Sekta ya Habari ikiwemo Maafisa Habari Wizara na Taasisi za Mradi kwa lengo la kuwapa uelewa wa mradi ili kusaidia katika usambazaji wa elimu na Matumizi Bora ya Nishati


"Mradi huu niwakutoa hamasa kuhusu matumizi bora ya nishati na kuleta manufaa makubwa nchini kwa kusaidia katika kupunguza matumizi ya nishati yasiyo ya lazima".Amesema Nyanda


Na Kuongeza" Kupitia Mradi huu utapunguza matumizi ya Nishati na kupata huduma ile ile kwani kama mtu alikua anatumia kilowat 10 kuzalisha kiasi cha bidhaa kwa kutumia Nishati ya Umeme sasa anaweza kutumia kilowat 5 kupata bidhaa ile ile kwahiyo kupitia jitihada hizi".Ameongezea 


Aidha amesema mradi huo unapunguza garama za nishati na hata kutekeleza jitihada za Taifa za utekelezaji wa Utunzaji Mazingira kwani inawezekana mtu anaweza kutumia Nishati nyingine inayotokea kwenye vyanzo ambavyo siyo rafiki wa mazingira.


Mradi unatekelezwa na Wizara ya Nishati kwa jukumu la uratibu mzima na maeneo mahususi yanayogusa Taasisi mbalimbali ikiwemo Shirika la Viwango TBS kusaidia kutambua Viwango vinavyoonyesha Matumizi Bora ya Nishati na kutambua viwango vya chini katika bidhaa zinazotumia Nishati kubwa.


"TBS watatusaidia kuja kuonyesha tunavyosema Matumizi Bora ya Nishati ni Viwango gani sasa vinaonyesha huo ubora mfano fridge ni nini kiwango cha chini kifaa kinatakiwa kuwanacho kwenye Viwango ambavyo vinatumia nishati ya chini na kupata ubora ule ule". Ameeleza


Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) watasaidia Katika masuala ya Ufundishaji wa wataalamu ambao watakua wasimamizi na wakaguzi wa Nishati."Tutaanza kuwafundisha ili kutembelea na akikuta matumizi yamekua juu ya kiwango atafanya ushauri kwamba umezidisha na akakupatia hatua zipi za kuchukua.


Aidha Taasisi ya Takwimu ya Haraka NBS washiriki katika uchukuaji wa Takwimu za Matumizi Bora ya Nishati.


Kadhalika Wizara ya TAMISEMI, Ewura, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mradi utawasaidia katika kuja na Mifumo, Miongozo ya Matumizi Bora ya Nishati husisani Majengo.


TIRDO Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania watakao saidia kushauri Matumizi ya Nishati Bora katika vifaa na kusaidia wale watakaopeleka vifaa kuchunguzwa kama vinakidhi Viwango vya Matumizi Bora.


Akitaja Maendeneo ya Kipaumbele ambayo yatasaidia kufikia lengo la Matumizi Bora ya Nishati ni pamoja na Viwango, Sheria, Mikakati na Uelimishaji ambapo mlengwa ni mwananchi."Tumefanya haya yote ikiwemo programu mbalimbali za utekelezaji na tunaposema mlengwa ni mwananchi ni kwasababu tutakua na Viwanda na hata wananchi ni Viwanda hivyo kutokana na juhudi zote hizi mwananchi atakua amepunguza matumizi ya Nishati mfano katika suala la taa kwamba kutokana na wananchi wengi kulalamilia unit za umeme zinaisha haraka kumbe inawezekana vifaa anavyotumia vinatumia umeme mwingi pasipo ulazima".Alieleza


Kupitia Mradi huo kutakua na kuingilia Kati kutambua vifaa labda vimetengenezwa Tanzania iwe balbu au nyaya kama vinatoa huduma za Nishati kwa viwango vya chini na huduma zile zile.


Amesema Miongozo itakayo andaliwa itawaongoza wananchi na kuwapatia elimu kwamba balbu yenye matumizi mazuri ya nishati kama haitumii umeme mwingi.


"Miongozo itakuja kwamba yeyote anayetengeza au anayeingiza Balbu ziwe za kiasi hiki ili tumsaidie mwananchi wetu".Amebainisha

 

Pia Nyanda amesema orodha ya vifaa vitakavyopewa Kipaumbele itatolewa kufuatia ushauri kutoka kwa Mshauri Elekezi ambaye atazunguka kwa wadau muhimu kukusanya maoni ya vifaa gani vya kupewa vipaumbele vya kuanza navyo ambapo wadau hao ni pamoja na Serikali, Watu binafsi, Viwanda, na Sekta mbalimbali.
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: