Na John Walter-Manyara

Wakala wa Bara bara za mijini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Manyara wanatarajia kutumia shilingi Bilioni 20.216 kwa mwaka wa fedha wa 2023-2024.

Kaimu Meneja wa TARURA mkoa wa Manyara Mhandisi Erick Chenga ameliambia baraza la ushauri la Mkoa wa Manyara (RCC) lililoketi leo Machi 19,2023 kuwa kwa bajeti hiyo,  wanatarajia kujenga lami kilomita 6.5 katika wilaya ya Simanjiro, Babati, Hanang’ na Mbulu. 

Kwa bajeti hiyo watafanya matengezo ya bara bara ya kawaida na muda maalum kilomita 940.17.

Pia watafanya ujenzi barabara za udongo kwa kiwango cha Changarawe kilomita 241.37, kujenga vivuko 40, daraja moja kubwa na madaraja madogo na saizi ya kati 26 na kufanya ukarabati madaraja mawili.

Share To:

Post A Comment: