Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohammed Mchengerwa wakishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohammed Mchengerwa wakishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani.Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohammed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Aboubakar Kunenge akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) Mhandisi Rogatus Matavila akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani.Viongozi wa Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani. Watumishi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) wakiwa katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani. Baadhi ya wahandisi wakiwa katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami uliofanyika leo Machi 19, 2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***************************

NA EMMANUEL MBATILO NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

Wakati leo Rais wa Jamhuri ya Muungano anapongezwa na Wanawake wote kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) historia inaandikwa kwa Serikali yake kutia saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) na daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami.

Ambapo Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) wameingia mkataba na Kampuni ya China Railways Seventh Group Limited kutekeleza ujenzi wa barabara ya Utete -Nyamwage km.33.7 pamoja na Kampuni ya Nyanza Roads Works katika ujenzi wa daraja la Mbambe.

Zoezi hilo limefanyika leo Machi 19,2023 katika Viwanja vya Azimio Utete Rufiji mkoani Pwani huku Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohammed Mchengerwa kushuhudia zoezi hilo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mhe. Mchengerwa ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage na amewaomba wakandarasi waanze ujenzi kwa kuanzia Utete hadi Nyamwage badala ya kuanzia Nyamwage kwenda Utete.

Mchengerwa amesema wanaRufiji walisubiri kwa kipindi chote ,na Sasa wanaishukuru Serikali kwa maendeleo yanayofanyika na kwenda Kuwa kitovu Cha maendeleo kupitia ujenzi wa miundombinu.

"Walipita viongozi mbalimbali kwa nyakati tofauti,na kila mmoja kuipigania Rufiji kadri ya uwezo wake na leo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka miwili kutuletea Neema hii ya barabara ya Utete -Nyamwage kwa zaidi ya Bilioni 67" Amesema Mhe.Mchengerwa.

Nae Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema gharama za ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage na Daraja la Mbambe zitagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 wakati miradi yote itagharimu zaidi ya sh.Bilioni 67 hadi kukamilika kwake.

Aidha Mhandisi Kasekenya ameiagiza TANROADS kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha.

Amesema ujenzi wa miundombinu inaendelea kujengwa na kutanua mtandao wa barabara nchini ambapo hadi sasa zimeshajengwa km. 11,000 huku km.24,000 zikiwa bado zinahitaji lami.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) Mhandisi Rogatus Matavila amesema upembuzi yakinifu wa barabara hiyo ulianza 2014 ambapo kutokana na muda kupita 2019 usanifu ulipitiwa upya .

Ameeleza kuwa zabuni ilitangazwa Sept mwaka 2022 na kufunguliwa November 2022 na baada ya tathmini kukamilika ilishinda Kampuni ya China Bil 43.4 bila VAT na itajengwa kwa muda wa miaka miwili.

Akielezea kuhusu ujenzi wa Daraja la Mbambe Mhandisi Matavila amesema kuwa Daraja la sasa limejengwa kwa mbao ni jembemba lenye njia moja ya kupita magari na halina uwezo wa kubeba magari yasiyozidi tani tano na Lina miaka 30.

Pamoja na hayo amesema Daraja litakalojengwa litakuwa na njia mbili na upana wa mita 7.5 na upana wa Jumla mita 10.5 ,nguzo mbili za pembeni mwanzo na mwisho wa Daraja kukutana na barabara zote ili kuwezesha kupanda juu ili lisiathirike na maji.

"Ujenzi huo utaenda Sambamba uwekaji wa alama za barabarani na kuweka taa za barabarani solar lights 18 ambazo zitasaidia kulinda usalama wa watumiaji nyakati za usiku." Amesema Mhandisi Matavila.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: