Kampuni ya Silverlands yenye makao makuu yake Mkoani Iringa imefungua tawi jipya la kutotolesha vifaranga Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Akizungumza wakati kiwanda kikianza kutoa huduma ya kutotolesha vifaranga na kuzalisha vyakula vya kuku Wilayani hapa Stanley Stephano Mtewele ambaye ndio meneja wa mradi huo amesema kuwa kwa wiki wana uwezo wa kutotolesha vifaranga takribani elfu 78.

Amebainisha kuwa uwepo wao Arumeru  kutarahisisha upatikanaji wa bidhaa ya kuku kwa mikoa inayopakana na Mkoa wa Arusha ikiwemo Mkoa wa Kilimanjato,Manyara,Dodoma ,Tanga na Dar es Salaam kuweza kufika kwa haraka ambapo amewataka wananchi kutegemea kupata bidhaa ya kuku kwa wingi  ikiwemo mayai.

"Tumeona tuongeze uzalishaji wa zao la kuku kwa walaji na kuwaondolea upungufu wa bidhaa hiyo ndiyo maana tumeamua kuongeza uzalishaji pindi uhitaji unapokuwa mkubwa tusiingie kwenye ukame wa bidhaa ya kuku nchini."alisema Mtewele

Aidha amesema kuwa kampuni hiyo inajihusisha na uzalishaji wa aina 3 wa vifaranga ikiwemo aina kuku wa mayai,kuku wa nyama na kuku chotara au saso,uwepo wa tawi hilo jipya katika Wilaya ya Arumeru ni kuweza kuwafiki wateja wa kaskazini kwa karibu zaidi kwasababu zao la kuku ni zao pendwa duniani kote .

Stanley aliongezea na kusema Takribani asilimia 85 ya watanzania katika mikoa yote Nchini hujihusisha na kilimo cha mazao hali inayopelekea kupungua kwa nguvu kazi ya ufugaji na kusababisha kushuka kwa soko na wakati mwingine kupungua kabisa.

Hali hiyo hutokana na watu wanaojihusisha na kilimo baadhi yao hujihusisha pia na ufugaji ambapo katika nyakati za kuanza kilimo asilimia kuwa ya wananchi ambao ni wafugaji pia huingia katika kilimo.

Kwa upande wake Afisa mauzo wa Kampuni Silverlands Mkoa wa Arusha, Ramuno Rashidi Ibrahimu amesema kuwa wafugaji wengi wanafuga vifaranga visivyokuwa na ubora hali inayopelekea kushambuliwa na magonjwa ikiwemo ugonjwa wa gomboro, ndui na magonjwa mengine ambukizi.

Ameongeza kuwa kwa kufungua kiwanda hicho wataweza kudhibiti magonjwa hayo kutokana na uwepo wa chanjo za kisasa ambazo hutumika katika kuzuia magonjwa hayo.

"Kwa Wilaya zetu kama wilaya ya Meru ,Monduli ,Arusha Mjini na wilaya nyingine ambazo zipo Arusha magonjwa haya yatakuwa ni baibai na kifaranga ambacho kitatoka hapa kitakuwa ni kifaranga chenye ubora na imara katika ufugaji."alisema

Amesema uwepo wa mradi huo wa kuku ndani ya kampuni hiyo kutaleta hamasa kubwa na chachu ta maendeleo kwa kila mmoja aliyeko ndani na nje ta nchi.

Lengo la mradi huo ni kumnyanyua mfugaji wa chini aliyeko ndani ya nchi kwa kipata bidhaa kwa bei nafuu ambapo amesema mbali na hilo kipo chuo ambacho kinatoa mafunzo ya ufugaji wa kisasa huku lengo kubwa likiwa ni kuunga mkono serikali ambayo siku zote inahimuza uwekezaji wa ndani nili kuweza kumuinua mfugaji wa chini na kufika katika kiwango cha juu kimaisha.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Meru ,Gurisha Sifael Mfanga amesema kuwa kama chama wamefarijika kuona mradi huo kuletwa katika Wilaya hiyo na kunufaisha wananchi katika kuhakikisha wanapata kuku walio bora na kupata fedha kutokana na mauzo yatokanayo na mradi huo.

Ameongeza kuwa mkulima au mfungaji hatopata shida kutokana na kampuni hiyo, kuwa kampuni ambayo inatotolesha vifaranga na kuzalisha vyakula vya kuku.

"Ninaona wazi kuwa mradi huo utakuwa mradi endelevu na utasaidia sana katika wilaya yetu ya Meru."alisema Katibu wa CCM Mfanga

"Katika utekelezaji wa chama cha mapinduzi,mradi huu ni moja ya utekelezaji wa chama cha mapinduzi kwa namna moja au nyingine na kusaidia vijana wetu kupata ajira   nikiwa na maana kwamba vijana tulionao kupitia ofisi ya mkurugenzi zile asilimia zinazotolewa za mikopo zitasaidia kuwapa vijana na kuweza kupata elimu ya kutosha katika ugugaji mzima wa kuku."aliongeza  Katibu wa CCM Meru


Share To:

Post A Comment: