Wa kwanza kushoto ni mkaguzi msaidizi wa Polisi Frank Mwanisi na mwa mwisho kulia ni OCD wa wilaya ya Nachingwea mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha akikagua timu kabla ya mechi za Mashindano ya Polisi jamii cup yakiendelea wilaya ya Nachingwea.
Mechi ya kimashindano ikiendelea



Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

WANANCHI wa wilaya ya Nachingwea wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha Mashindano ya Polisi jamii ambayo yenye lengo la kuendeleza mahusiano mazuri na Jeshi hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Polisi jamii wilaya ya Nachingwea, mwenyekiti wa waendesha pikipiki (bodaboda) wilayani Nachingwea Hashim Awadhi alisema kuwa lengo la Mashindano hayo ni kuimarisha mahusiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi.

Awadhi alisema kuwa Polisi na wananchi wakiwa na mahusiano mazuri vitendo vya uharifu vitapungua kutokana na Jeshi hilo kupata taarifa Mara kwa Mara kutoka kwa raia wema.

Alimazia kwa kumpongeza OCD wa wilaya ya Nachingwea James Chacha kwa kuwa na mahusiano mazuri na wananchi Jambo ambalo limesaidia kupunguza vitendo vya uharifu wilaya ya Nachingwea.

Kwa upande wake OCD wa wilaya ya Nachingwea mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha alisema kuwa lengo la Mashindano ya Polisi jamii ni kuimarisha mahusiano na wananchi wa Nachingwea.


Chacha alisema kuwa wameanzisha Mashindano hayo kwa kuwashirikisha vijana zaidi kwa kuwa kundi hilo ndio limekuwa linatumika kufanya vitendo vya uharifu mtaani.


Alisema kuwa ukitoa elimu ya madhara ya uharifu kwa jamii kupitia vijana basi hapo baadae kutakuwa na kizazi bora ambacho kitakuwa tayari kupambana na uharifu wowote ule.

Chacha alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia Mbuzi mmoja,ya jezi seti moja na mpira mmoja, mshindi wa pili atapata jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa tatu atapata jezi seti moja.

Hivyo Mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha kuomba wananchi kujitokeza kwenye mechi za Mashindano hayo ili kupata elimu mbalimbali kutoka kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: