👉Atoa wito kwa wananchi kuitumia

Na John Mapepele

Serikali imewataka wananchi wote nchini kutumia boti ya kisasa ya Utalii iliyozinduliwa rasmi leo ili kukuza utalii wa ndani.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa Kilwa Masoko kwenye hafla ya uzinduzi wa boti maalum ya Utalii ijulikanayo kama TAWA SEA CRUISER inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa boti hiyo itakuwa ikifanya safari katika ukanda wote wa Pwani ili wajionee vivutio mbalimbali vya utalii.

Amevitaja baadhi ya vivutio vya utalii vinavyopatikana katika eneo la Kilwa kuwa ni pamoja na misitu ya matumbawe, kasa, mikoko, na samaki wa aina mbalimbali.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ametembelea maeneo ya kitalii ya mji mkongwe wa kihistoria wa Kilwa na kujionea vivutio vya utalii vya asili kama msikiti wa Karne ya 12 magofu ya kale na jumba la mfalme.

Akiwa katika msikiti wa kale ameiagiza Bodi ya TAWA kuona namna ya kuboresha mji huo ili kuvuta watalii wengi.

Pia Kisiwani hapo Mhe Mchengerwa ameshuhudia boti ya kisasa ya Le Jacques Cartier Ponant kutoka nchini Ufaransa ikitia nanga katika fukwe ya Kilwa Kisiwani na baada ya muda mfupi kuanza kuwashusha wageni.

Boti hiyo ni ya tatu katika kipindi cha wiki moja tushusha wageni ambapo boti ya kwanza ya Coral Geographer kutoka Australia ilishusha wageni 120 Machi 7 mwaka huu ikafuatiwa na Meli hii hii Machi 9 iliyoshusha pia watu 110 na hii ya leo iliyoshusha wageni 93 kutoka nchini Ufaransa.   
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: