Denis Chambi,  Tanga.

MTEGO uliowekwa na jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga umefanikiwa kuwanasa Mawakala wanne waliokuwa wanajihusisha na biashara haramu ya usafirshaji wa binadam waliokuwa wamewahifadhi katika nyumba ya mmoja wao iliyoko Muheza mkoani Tanga .

Akizungumza na waandiahi wa habari ofisini kwake  kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga  Kagimbo Bakari amesema kuwa kwa kipindi cha muda  wamekuwa wakipambana kuweka mbinu mbalimbali z kuweza kuwabaini wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo ambapo wamefanikiwa kuwakaata na tayari wamefikishwa mahakamani.

Amewataja mawakala hao kuwa ni Joseph Thimothi mwewnye nyumba walimokuwa wamehifadhiwa wahamiaji hao,  wengine ni  Charles Mwapela Kimaki Maneno,  Athuman  Mwameja pamoja Majoka Kipala wote hawa wakiwa ni raia wa Tanzania.

"Hawa  ni mawakala ambao wanahusika na usafirishaji  haramu wa binadamu karibu nyakati zote tumekuwa tukipambana kutafuta  mawakala na tumewapata kutokana na mahusiano ya kesi ambazo nyingine ziko zinaendelea mahakamani  na watuhumiwa wote tumewafikisha katika ofisi ya uhamiaji mkoa wa Tanga na mahojiano bado yanaendelea" alisema Kamanda Bakari

Aidha katika taarifa nyingine Jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga march 10, 2023 limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haram wanne raia wa Cameroon katika nyumba za kulala wageni jijini hapa wakidai kuwa wamekuja  kwaajili ya kufanya mazoezi ya  kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports ambapo wameletwa  na wakala wao  aliyefahamika kwa jina la Benard Matomondo Mfaume.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga Kagimbo Bakari alieleza kuwa raia hao ambao waliingia hapa nchini kupitia  uwanja wa Ndege wa  Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na hatimaye kufanikiwa kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90 badala ya visa za kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.

"March10, 2023 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya New MayLodge na New Palm Life  zilizopo jiji la Tanga barabara ya 4 na  20  walikamatwa raia wanne wa Cameroon walikuja mkoa wa  wanavyodai wao wamekuja katika timu za Coastal Union na African Sports kufanya mazoezi ili kujiunga na timu hizo  kwa msaada wa wakala wao wa michezo aitwaye Benard  Mtomondo Mfaume anaishi Dar es salaam"

"Uchunguzi wa awali unaonyesha  raia hawa wa Cameroon waliingia kupitia  uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JKNIA na kupata viza za matembezi ya siku 90  na sio za kufanya shughuli zozote za michezo na wapo hapa tayari kwa kufanya mazoezi ili waweze kisajiliwa katika timu hizo za Coastal Union na African Sports" alisema Kamanda Bakari.

Hata hiyo kamanda huyo alibainisha kuwa mara baada  ya kuwakamata raia hao waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal ambao walikanusha kutokuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua walizokuwa nazo zote ni za kughushi na paspoti walizokuwa nazo sio sahihi.

"Uchunguzi uliofanyika katika timu ya Coastal Union kupitia kwa katibu wa klabu  anaeleza kutokuwatambua wala kuwafahamu na wala hana mawasiliano nao  kwa mfano barua zote walizonazo ni za kughushi  sii barua sahihi na paspoti walizo nazo sio paspoti sahihi kwa mujibu wa viongozi wa Coastal Union kwamba hawajawahi kuwaona wala hawahusiki nao" 

"Kwa upande wa African Sports  wao wameeleza kutokuwatambua na kwamba wana barua ya Fountain Get na Pamba Football klabu bado wakala wao wa michezo tunaendelea kumtafuta kwani hapokei simu ili tuweze  kujua   anaye wahudumia hapa mkoani Tang alielezaKamanda huyo.

Aliwataja majina raia hao kuwa ni Romanus Gwa,  Cedric Donald Pouanguae Tchchoua, Sainsburunde Nji,  pamoja na RowandBenard Messi Tangana.
Share To:

Post A Comment: