Akishiriki katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha 18 cha maafisa habari mawasiliano na uhusiano serikalini Jijini Dar es salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Sophia Edward Mjema ameelekeza  Maafisa Habari kujizatiti kwenye mawasiliano ya Kimkakati katika kueleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

"Maafisa habari wa serikali ni wajibu wenu kutoa Taarifa za miradi inayotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kufahamu ni nini serikali inafanya kuwaletea Maendeleo."

Chama Cha Mapinduzi Kitaendelea kusimamia na Kufuatilia ufanisi wa mawasiliano kwa umma baina ya Serikali na Wananchi.

Share To:

Post A Comment: