Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepewa jukumu la kusafirisha misaada iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jamhuri ya Malawi iliyoathiriwa na Kimbunga 'Tropiki Freddy'.


Akitoa ufafanuzi leo machi 18, 2023 Jijini Dodoma, Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema misaada hiyo inahusisha vyakula, mahema na misaada mingine ya kibinadamu.


"Kufuatia maafa ya kimbunga nchini Malawi, Serikali imeamua kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ili kuisaidia nchi jirani, JWTZ imepewa jukumu la kusafirisha misaada hiyo. 


"Tunatarajia shehena zitaondoka muda wowote kuanzia sasa, jumla ya tani 1,000 za unga wa mahindi zitasafirishwa kwenda Malawi, amesema tani 90 zitaondoka kila siku zikitokea Dodoma.


"Tani 60 za unga wa mahindi zitaondoka kila siku kutokea mkoani Iringa, mablanketi 6,000 yataondokea Dodoma, mahema yasiyopungua 50 yataondoka yakitokea jijini Dar es Salaam," ameeleza Luteni Kanali Ilonda.

 

Ikumbukwe kuwa machi 13,2023 Kimbunga kilichoambatana na mvua kubwa na upepo mkali kiliikumba nchi ya Malawi kiasi cha kutangazwa kuwa janga chini humo baada ya kusababisha Vifo, Kuharibu Miundombinu, Nyumba, Mazao na athari zingine. 


Luteni Kanali Ilonda amesema kufuatia janga hilo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitambua ujirani mwema, Ushirikiano na Udugu wetu na nchi ya Malawi imetoa misaada hiyo ili kusaidia nchi hiyo kukabiliana na janga hilo.


Aidha amesema kufuatia jukumu waliyopewa Jeshi la Wananchi wa Tanzania La kusafirisha misaada hiyo Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda, ametoa maelekezo yaliyoratibiwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Ambapo ni Magari ya JWTZ zaidi ya 37 yatakayo ondoka Dodoma muda wowote kuanzia hivi sasa kupeleka misaada nchini Malawi.


Baadhi ya magari hayo yanayopelekwa malawi ni pamoja na gari la Wagonjwa (Ambulance), Karakana ya magari inayotembea (Mobile Workshop), Malori makubwa yenye uzito wa tani 30 yapatayo (20) na Malori yenye uzito wa tani zaidi ya kumi na nane 18 yakiwa (10). Amesema Luteni Kanali Ilonda


Magari hayo yatasafirisha msaada wa Mahema, Mablanketi, Chakula na Mahitaji Mengine ya kibinadamu yaliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sambamba na Hilo Amesema Katika maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Majeshi ameelekeza Helikopta za Jeshi zitumike kama sehemu ya msaada uliotolewa na Serikali kusaidia Nchi ya Malawi kukabiliana na Maafa Yaliyoikumba.


Hivi punde Helikopta Mbili (2) za kijeshi zimeruka kutokea Dear es salaam kuelekea nchini Malawi tayari kuanza utekelezaji wa majukumu hayo. Amesema




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: