Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto
Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto
Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkurugenzi wa Msowoya Foundation, "Dkt Tumaini Msowoya"ameikumbusha jamii kuhusu malezi ya watoto.

Amesema mmomonyoko mkubwa wa maadili unatokana na malezi hafifu ya baadhi ya wazazi na walezi kutokana na ubize wa kazi bila kukumbuka watoto wao.

Akizungumza na wananchi wa baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Kilolo, Dkt Msowoya amesema watoto wanaweza kuwa salama ikiwa watalindwa na kufundishwa maadili mema.

"Kuna haja gani kwako kuwa bize wakati mtoto wako anaharibika? anafanyiwa ukatili wala huna habari? ukirudi nyumbani hoi hata muda wa kuongea nae huna, tubadilike ndugu zangu. Tukienda shambani basi tukumbuke tuna watoto," amesema na kuongeza;

"Sisi Msowoya Foundation tutaendelea kutoa elimu kwa jamij yetu, malezi ya watoto ndio ambayo yanaijenga kesho yenye watu wastaarabu na wenye utu," amesema.

Dkt Msowoya ni mwanaharakati wa haki za watoto, mwimbaji wa muziki wa Injili, mwanahabari nguli na mwanasiasa akishika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: