Na John Walter-Babati

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA  kimefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Ayalagaya,  Dareda kati wilaya ya Babati mkoani  Manyara, mkutano uliogubikwa na kampeni za katiba mpya na kukiondoa madarakani chama tawala.

Viongozi wa chama hicho kila aliepanda jukwani alisisitiza kuwa wamejipanga kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu 2025  ili watatue changamoto zinazowakabili Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo Machi 11,2023 Naibu Katibu Mkuu Bara  Benson Kigaila,  amesema  wamejiandaa kupambana kushinda chaguzi zote.

Amesema ni wakati wao kuongoza nchi kwa kuwa chama Cha Mapinduzi kimeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake ndani ya miaka 62 licha ya kuwa na utajiri wa kila aina ya madini.


Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi,   amesema sababu ya kuomba katiba mpya ni pamoja kuwaondoa wakuu wa wilaya na mikoa ambao wanatokana na uteuzi.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Manyara Derick Magoma amesema "hatuwezi kuwa na viongozi wale wale,wa chama kile kile, wa sera zile zile miaka nenda rudi, 2025 ama zao ama zetu, hawachomoki"

Mgombea Ubunge katika jimbo la Babati Vijijini kupitia tiketi ya CHADEMA Mathayo Gekul amesema kwa sasa ndo wameanza rasmi ratiba ya mikutano yao na watapita kila kata kuwaelimisha wananchi kuhusu katiba mpya.

Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na Aisha Madoga kutoka jijini Dodoma, Emmanuel Ntobi wa Shinyanga, Asenga.

Share To:

Post A Comment: