. Na Bakari Madjeshi,

Mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Osam Milanzi, mkazi wa Dar es Salaam ambaye aligongwa na Gari la Mwendokasi wakati anatembea kwa miguu kandokando ya Barabara ya Morogoro na Jamhuri, ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), imeeleza kuwa Milanzi ameruhusiwa kutoka hospitali tangu alipofikishwa hospitalini hapo Februari 22, 2023 baada ya kutokea ajali hiyo maeneo ya Kisutu, Dar es Salaam.

“Milanzi alifikishwa MOI tarehe 22/2/2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika Kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A, alifika hapa akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia,” imeeleza taarifa hiyo ya MOI.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, Milanzi ataendelea na huduma kama mgonjwa wa nje na atarudi Kliniki baada ya wiki mbili tangu aruhusiwe kurudi nyumbani. Hata hivyo, MOI imetoa shukran kwa watanzania wote, Vyombo vya Habari ambao wameshirikiana nao katika kumuombea na kumtangaza Osam Milanzi hadi kupatikana kwa ndugu zake.

Osam Milanzi alikutwa na ajali hiyo, Februari 22, 2023 majira ya saa 6:10 katika makutano ya barabara ya Morogoro na Jamhuri, Kisutu, jijini Dar es salaam ikihusisha Gari namba T122 DGW Aina ya Dragon mali ya Kampuni ya UDART (Mwendokasi) na Gari ndogo aina ya Toyota Avanza, mali ya Rwanda Air
Share To:

Post A Comment: