Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda amesema Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejiondoa jukumu la kusema shule ipi bora lakini takwimu za shule ipi bora zipo na kila mtu anaweza kuzipata.

Profesa Mkenda alkuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Bunda Vijijini Mwita Getere aliyetaka ufafanuzi kuhusu minong’ono iliopo mitaani kuhusiana na NECTA kushindwa kutaja viwango vya ufaulu kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka 2022.

Getere aliomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge kwa kutumia kanuni ya 76 ya bunge na kutaka ufafanuzi kuhusu hatua hiyo ya Baraza la Mitihani la Tanzania kubadali utaratibu wake wa kutangaza matokeo kwa shule na wanafunzi bora.

Akijibu muongozo huo, Waziri Mkenda amesema kwa sasa watakua wakitumia mfumo wa kuangalia namna shule inavyoweza kuongeza elimu ya wanafunzi kutoka kiwango kimoja kwenda kiwango kingine na sio matokeo ya mwisho.

Profesa Mkenda amesema, pamoja na kuangalia viwango vya ufaulu lakini wataangalia pia mazingira ya kujifunzia ya mwanafunzi na shule ili kuona namna ambavyo hatua zimepigwa kuhakikisha mwanafunzi anafaulu licha ya mazingira ya kujifunzia kuwa magumu.Share To:

Post A Comment: