Na Magesa  Magesa,Arusha

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania imewataka madiwani viti maalumu
wa mkoani hapa wanaotokana na Jumuiya hiyo kutekeleza majukumu yao
kikamilifu ikiwa ni pamoja na kushiriki na kuhudhuria vikao vyote vya
Jumuiya na Chama kuanzia ngazi za matawi hadi mkoa.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha, Flora Zelothe, aliyasema hayo juzi
alipokuwa akizungumza na madiwani hao katika kikao maalumu
kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoani hapa ambacho kililenga
kukumbushana wajibu na majukumu.

Amewaambia kwamba wakati wa Uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake
uliofanyika mwaka jana,  kila mmoja alikuwa na mgombea alie muunga
mkono lakini chaguzi zikishamalizika makundi yote na kambi zote
zinavunjika na kinachobakia ni kutekeleza majukumu na kuchapa kazi kwa
pamoja ili kuhakikisha ikani ya CCM inatekelezwa kikamilifu.

Amesema Madiwani wote wa Viti maalumu wanatakiwa kfanya ziara katika
maeneo yao na kwamba wanatakiwa wawasiliane na uongozi wa jumuiya
wilaya ili wapewe ratiba na baada ya ziara hiyo watatakiwa kupeleka
taarifa ya ziara Wilayani na nakala Mkoani.

Nae Katibu wa UWT, Mkoa wa ArushaMwasiti Ituja, alisema kuwa Jumuiya
imeweka utaratibu ambapo kila baada ya miezi minne wanatakiwa wasome
taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya  Chama cha Mapinduzi
kwenye mikutano ya mabaraza ya madiwani katika halimashauri zao .

Amesisitiza kwamba ni lazima madiwani viti maalumu wafanye ziara
waeleze mazuri yote yanayotekelezwa na serikali inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan ili wananchi waelewe na hivyo kuepuka upotoshwaji
utakaotolewa na watu wengine

Katibu huyo wa  UWT Mkoa amewataka madiwani hao kuhakikisha kuwa
wanahimiza wanawake katika maeneo yao kujiunga na Jumuiya hiyo na
kwamba UWT Mkoa wa Arusha itatoa zawadi kwa wilaya ambayo itaongoza
kwa kuingiza wanachama wengi.

Share To:

Post A Comment: