Naibu Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Abdala Ulega Na Mbunge Wa Jimbo La Monduli Fredrick Lowassa Wajadili Ugugaji Bora Monduli.

 

Haya yanajiri katika ziara ya naibu waziri wa mifugo na uvuvi mh abdala ulega wilani monduli ya kukagua miradi ikiwemo ukuta wa mnada wa meserani pamoja bwawa la naalarami lenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni mia nne.

 

Awali akizungumza mbunge wa jimbo la monduli Frederick Lowassa ameanza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupendelea monduli kwa miradi mbalimbali za maendeleo.

 

Frederick Lowassa ameongeza kwa kusema kuwa swala la maji katika kata ya Naalarami ni tatizo kubwa lakini kupitia mradi mkubwa wa arusha wananchi wa naalarami wanaweza kunufaika na mradi huo.


 

"Hali ya maji na ukame hapa ni mbaya sana tunaongelea ukame nchi nzima , mabadiliko ya tabia ya nchi , hali ya ukame naalarami ni mbaya poleni sana ,natambua kilio chenu inauma kwelikweli "

 

"Huyu ni mbunge mkuranga na ni mvuvi lakini pia anapenda mifugo ,bungeni akisimama anajibu maswali vizuri za wabunge , sasa naibu leo umekuja monduli hapa tunachojua ni mifugo mifugo kwa hiyo hapa tuone namna bora ya kufuga kisasa na kuwavuna mifugo yetu." amesema Lowasa

 

Kwa upande wake Naibu Waziri Abdala Ulega amewataka wafugaji kubadilisha fikra ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,ambayo inatoka na ukame uliokidhiri na kuimbuka maeneo hayo.

 

"Lazima tuishi kwa maarifa tufanyaje unakuwa na kundi kubwa la ng'ombe elfu moja elfu mbili halafu wanakuja kusafishwa na ukame wote, ni hatari sana lazima tukubali kuwa kuna mabadiliko ya tabia ya nchi".amesema Ulega



 

Ameongeza kwa kuwataka wataalamu kuwasaidia wafugaji kufuga kundi dogo la ng'ombe lenye tija .

 

 

Wakati huohuo mkuu wa wilaya ya monduli selemani yusuph mwenda amesema wilaya ya monduli imepoteza mifugo mingi kutokana na ukame .

 

"Mifugo takriban laki moja na elfu 30 imepotea kati ya mwaka 2021 hadi 2023 na hili ni kutokana na mifugo kushindwa kuhimili ukame katika maeneo yetu" .amesema Dc Mwenda



Akizungumza kwa niaba ya Wananchi Oltus Olteyetu Mwanachi Kijiji cha Naalarami amekiri kuadhirika kwa ukame huo na kuwataka wataalamu wafike vijijini kutoa elimu ya namna bora ya ufugaji kisasa.



Share To:

Post A Comment: