Na;Elizabeth Paulo,Dodoma

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA umesema miongoni mwa changamoto zinazokabili wakala ni pamoja na Ulipaji wa huduma za magari na kurudisha nyuma maendeleo Yao kama wakala.


Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala wakati akizungumza na wanahabari juu ya majukumu mbalimbali ya TEMESA na utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa wakala huo kwa mwaka 2022/23.


“Miongoni mwa vitu ambavyo vinaturudisha nyuma sana ni ulipaji wa (washitiri) wale wateja wetu tunaowahudumia niwakusuasua kiasi kikubwa na madhara yake madeni yanakua Makubwa na tunashindwa kuwalipa wale wazabuni waliotuuzia vipuli sasa inatengeneza mzunguko wa matatizo kwasababu mzabuni naye akijua anakupa kifaa chake na hajui utamlipa lini anapandisha bei kwasababu anajua kuna ucheleweshaji hivyo kupelekea serikali inalipa zaidi kutengenezewa magari hivyo huo mzunguko hauna tija kwa upande wowote”.Alisema Kilahala


Amesema nivyema kushirikiana kuwakumbusha wahusika kulipa kwa wakati katika kuipunguzia serikali mzigo kwani hakuna tija yoyote serikali inapopandishiwa bei za juu kwasababu za kutokulipa kwa wakati. 



Kilahala amesema Kwa mujibu wa hesabu za mwisho Zilizofungwa 2021/2022 TEMESA inadai bilioni 44 kwa Taasisi mbalimbali za serikali na Wakala hudaiwa shilingi bilioni 48.


“Utofauti utaona tunadaiwa hela nyingi kuliko tunazodai kwasababu tunadaiwa pale tunapo pokea kifaa (spare) lakini tunadai pale tunapokua Tumetengeneza gari”.Alisema 


TEMESA ilitangazwa katika gazeti la serikali Na.254 la tarehe 26 Agosti,2005 na kuzinduliwa rasmi tarehe 23 juni ,2006 ambapo TEMESA ilikasimishwa majukumu yote yaliyokua yanatekelezwa na Idara ya Ufundi na Umeme (E&M Division) iliyokua chini ya wizara ya Miundombinu ili kuendelea kutoa huduma bora na endelevu zenye kuwaridhisha wateja.



Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: