Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wa pili kushoto akiongea na viongozi mbalimbali wakati wa kikao cha tathimini ya taaluma ya elimu wilayani humo.
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea walipohudhulia kikao cha tathimini ya taaluma ya elimu.
Na Fredy Mgunda Nachingwea.


MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuongeza ubunifu wa namna ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuifuta kabisa alama sifuri kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kikao cha tathimini ya taaluma ya elimu,mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa hataki kusikia mwanafunzi amepata alama sifuri kwenye matokeo yoyote yale katika wilaya ya Nachingwea.

Moyo alisema kuwa ameangalia kwa miaka mitatu hadi minne ya nyuma na sasa bado hali ya ufaulu ipo chini hivyo walimu na viongozi lazima waongeze maarifa ya kufundishia wanafunzi ili waweze kuongeza ufaulu na kufuta kabisa sifuri.

Alisema kuwa ametoka katika wilaya ya Iringa ambayo imekuwa ikishika nafasi za juu za ufaulu kila mwaka hivyo hataki kusikia wilaya ya Nachingwea inashika nafasi ya mwisho bali anataka juhudi ziongezeke ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

"Nimekuja hapa nikiwa na maono ya kukuza elimu ya wanafunzi wa wilaya ya Nachingwea na sitaki mchezo kwenye elimu hivyo mtu yoyote yule atakaye chezea sekta ya elimu atapata haki yake" alisema Moyo

Moyo alimazia kwa kuwataka viongozi wote ambao hajahudhulia tathimini ya taaluma ya elimu kufika ofisini kwake Mara moja kwa kosa la kutohudhulia kikao muhimu ya kujadili hali ya elimu ya wilaya hiyo.Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: