Mkuu wa TAKUKURU  Halmashauri Wilaya ya Bahi, Erick Kilawe  Amesema Programu ya  "TAKUKURU RAFIKI"imeanzishwa Maalumu kutoa fursa kwa kila Mtanzania kushirikiana na Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo ni kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Hayo yamejiri Jijini Dodoma Wilaya ya Bahi wakati wa Uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU RAFIKI ambayo inazinduliwa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Wilaya na kata huku akisema programu inaakisi maana ya rafiki kwa kubeba dhana ya kuwa karibu na ushirikiano wa dhati kwa kila mwananchi na wadau.

“Hii itatekelezwa kwa kuwa na vikao katika ngazi ya kata kwa lengo la kutambua kero zilizopo kwenye utoaji au upokeaji wa huduma kama za Afya au Elimu pamoja na mchakato wa kutekeleza miradi ya maendeleo ujenzi wa miundombinu ya maji, Wadau wa kufumbua vitendo vya Rushwa ni pamoja na wananchi naomba tushirikiane ukiona kuna dalili yoyote ya Rushwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo toa taarifa”. Alisema Kilawe
Mchunguzi mkuu Takukuru Emmanuel Masawe Ametoa wito kwa Wananchi na wadau kushirikiana kuzuia vitendo vya Rushwa katika utoaji wa huduma kwa umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Programu ya "TAKUKURU RAFIKI".

“Usikae pembeni tushirikiane katika hili kwa pamoja tunaijenge Tanzania”.Alisema Masawe

Aidha Mhe.  Diwani kata ya mpamatwa ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuwapatia semina namna ambavyo taasisi hiyo inavyofanya  kazi kwa karibu na wananchi katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya rushwa.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: