Na; Elizabeth Paulo, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema Serikali itaanza mara Moja uwekaji wa kamera barabara kuu ili kusaidia ufuatiliaji wa Magari na madereva wanaovunja sheria za usalama wa barabarani.

Masauni amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa Habari jijini Dodoma, mara baada ya kutokea kwa ajili iliyopoteza maisha ya watu 12 wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma na ajali ya Korongwe Mkoani Tanga tarehe 3/2/2023 huku akisema Serikali haiwezi kukaa kimya ikiona wananchi wake wakipoteza maisha na wengine wakipata ulemavu wa maisha.


Amesema uchunguzi wa awali unaonyeasha sababu kubwa ambayo ni Uzembe wa baadhi ya madereva waliopewa dhamana ya kuendesha Magari wakikosa nidhamu katika kazi zao nakwamba ajali zote hizo zimesababishwa na mwendo kasi wa Magari.


Aidha amesema baada ya kugundua sababu hiyo Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuangalia mfumo wa utoaji leseni nchini unaohusisha sekta tayu ambayo ni pamoja na Ufundishwaji au Elimu inayotolewa kwa madereva, Jeshi la polisi dawati la leseni, Na Dawati la leseni TRA ili mfumo wa utoaji leseni unasomana.


Kadhalika amesema uhakiki wa madereva unaanza kuanzia leo hususan madereva wa Mabasi na Malori ili madereva wote wasajiliwe na latra na dereva asiyepita katika mfumo huo hataruhusiwa kuendesha gari aina yoyote iwapo atabainika sheria Kali zitachukuliwa dhidi yake.




Waziri huyo ametoa Wito kwa wamiliki wote wa magari kuhakiki madereva wao wanapotoa na mmiliki inapotokea ameruhusu dereva ambaye Hana vigezo na yeye atakua ameshiriki kwenye uhalifu huo.


Masauni amesema katika kuwafuatilia madereva madereva wote barabarani Serikali itaongeza maaskari katika barabara kubwa zote na kuomba ushirikiano kwa wananchi kutoa taarifa yoyote ya vitendo vya rushwa barabarani.


Kwa upande Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika ametoa leseni bila kufuata utaratibu aidha kuwaadhibu wale wote wanaotoa na kupokea rushwa ikiwemo polisi wanaopokea rushwa huku akisema wanachafua taswira ya Jeshi la Polisi na Serikali.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: