Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa wakiongozwa na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mheshimiwa Mizengo Pinda wakizindua ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo.
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa Ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Peres magili akitoa taarifa ya ujenzi wa Ofisi hiyo.
Hii ndio ofisi ilivyojengwa na MNEC Salim Asas wilaya ya Kilolo.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mlezi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa na Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda amempongeza MNEC Salim Abri Asas kwa kuendelea kukiimarisha chama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kilolo, Pinda alisema kuwa asilimia 85 za ujenzi wa ofisi hiyo imechangiwa na MNEC Salim Asas hivyo wanaccm wanatakiwa kuendelea kushirikiana na MNEC huyo ambaye amekuwa akijitoa katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa chama hicho mkoa wa Iringa na nyanda za juu kusini.

Pinda alisema kuwa MNEC Salim Abri Asas amejenga ofisi bora na mfano Tanzania nzima kwa ofisi za chama ngazi ya wilaya na kuwataka wanachama wa CCM kuiga mfano wa Asas katika kukiimalisha chama hicho mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa wanaccm wanatakiwa kuwa na  umoja,mshikamano katika kukiimalisha chama hicho akikitaka kisiwapuuze viongozi wake waliomaliza muda wao wa uongozi.

“Uongozi ni kupokezana vijiti, waliondoka madarakani tusiwapuuze; tuwaheshimu na tuwatumie, hao sio maadui wa chama ni sehemu yetu,” alisema.


Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Ofisi hiyo, mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Peres Magiri alisema kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi, Salim Asas ametumia Sh Milioni 151 kati ya Sh Milioni 179.6 kukamilisha ujenzi wa ofisi ya chama hicho ya wilaya ya Kilolo.

Magiri alisema kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo iliyozinduliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mizengo Pinda kunakamilisha ndoto ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo kwa kuwatoa katika jengo chakavu walilokuwa wakilitumia awali na kuwaongezea ufanisi wa kazi kwa watendaji wa chama hicho.

Pamoja na ujenzi wa ofisi hiyo, Asas ametoa ahadi ya kujenga ofisi zake zitakazokuwa za kisasa katika kata zote 106 za mkoa huo wakati  wa maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya chama hicho yaliyofanyika kimkoa wilayani Kilolo.

Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa MNEC Salim Asas alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanajenga ofisi za kata zote ili chama hicho kinatakavyo timiza miaka 50 CCM Iringa watakuwa hawana tatizo la ofisi za kata za chama hicho.

Asas alisema kuwa ofisi hizo zitakazojengwa ndani ya miaka mitano ijayo kwa gharama ya kati ya Sh Milioni 20 na Sh milioni 50 imekuja huku akiwa tayari amejenga ofisi ya kisasa ya chama hicho katika kata ya Kiyowela wilayani Mufindi iliyogharimu zaidi ya Sh Milioni 51.

“Baada ya kuzindua ofisi hii ya wilaya, nikuahidi Mheshimiwa Pinda kwamba tutaendelea kukuita mkoani kwetu kuzindua ofisi tutakazojenga katika kata zote za mkoa wa Iringa, kazi nitakayofanya kwa kushirikiana na wanachama na viongozi wenzangu. Kwa hiyo usichoke,” Asas alisema.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: