Na Denis Chambi,  Tanga.

Kongamano la kutokomeza maadili potofu kwa watoto litakalohusisha madhehebu mbalimbali linataraiwa kufanyika jumamosi hii katika viwanja vya Pongwe jijini Tanga hii ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa  maendeleo  pamoja na serikali katika kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi  kwa  watoto ndani ya  jamii.

Kongamano hilo litaambatana pia na zoezi la upandaji wa miti katika viunga hivyo ikiwa ni kuhamasisha jamii juu ya  utunzaji wa mazingira ili kuepukana na athari mbalimbali  ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza muandaaji wa kongamano hilo ambaye pia ni mchungaji wa  kanisa la Tanzania  Assembly of God 'TAG' mtoto wa simba wa kabila la Yuda  na mwalimu wa  mtoto mashuleni Agnes Willium alisema  masuala ya malezi ya kiimani kana kwamba yametupiliwa mbali na jamii  hivyo kupelekea  janga la mmomonyoko wa maadili hasa kwa watoto  wengi kufanyiwa vitendo vya ukatili jambo ambalo linakiuka taratibu na haki za kibinadamu huku viongozi wa dini nao wakihusishwa katika kutekeleza vitendo hivyo.

Alisema ni matarajio makubwa kama jamii inaweza kubadilika ikishirikiana kwa pamoja na juhudi za serikali pamoja na wadau mbalimbali  wa maendeleo huku akielekeza  zaidi kuwalea waoto ambao ni taifa tegemezi la kesho kupitia malezi ya   kiimani ambayo yatachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya ukatili.

"Kongamano hili ni la dini zote na watu wote , Lengo kubwa ni kwaajili ya kutokomeza maadili potofu kwa watoto jamii ipate elimu kwa sababu wapo viongozi wa dini nao pia wanasababisha mmomonyoko wa maadili  kutakuwa na maswala ya maadili,  kujitambua kwa mtoto ili aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali ,  na kufundisha kuhusu hofu ya Mungu ambayo ukiwa nayo huwezi kutenda dhambi sambamba na kupanda miti lakini kikubwa zaidi ni kutokomeza mmomonyoko aa maadili kwa watoto wetu hatimaye waweze kuwa na kizazi kizuri"

"Kuhusu kutokomeza ukatili wa watoto na wanawake  tukiwa na maadili ya  dini itasaidia sana lakini tuna maeneo matatu muhimu ambayo ni mzazi mwenyewe shuleni anakosoma pamoja na mafundisho ya dini akifundishwa vizuri anaweza kuwa mtu mzuri kabisa baadaye" alisema Mchungaji Agnes.

Share To:

Post A Comment: