Na Joel Maduka Geita..

Mmbunifu wa mitindo ya mavazi Kutoka Mkoani Geita,Bertha Joseph Komba(KASIKANA) Anatarajia kuzindua Jukwaa la Golden Fashion Festival  ambalo linalengo la kuibua vipaji mbali mbali vya wabunifu pamoja na kuhimiza jamii kuipa thamani biashara ya ubunifu  kwani bado jamii kubwa hapa nchini imekuwa ikipuuzia kazi mitindo hasa ushonaji kwa kuona kazi hiyo aina manufaa makubwa.

 

Akizungumza na waandishi wa Mmbunifu wa mavazi Bertha Komba alimaarufu Kasikana Collectione amesema ameamua kuja na jukwaa la Golden Fashion Festival kwa lengo la kuibua na kutangaza vipaji vya wabunifu kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na kuipa thamani kazi ya  ubunifu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikikosa sapoti kutokana na kuonekana   ni kazi ya masirahi kidogo.

“Tunaimani kupitia jukwaa hili tutaiomba Serikali kuitazama kwa jicho la kipekee Sanaa ya ushonaji na ubunifu kwa waweze kuiongezea thamani hasa katika matumizi yam ashine za kisasa ,lakini pia iweze kuboresha vyuo vya ufundi na kujenga viwanda vya ushonaji ambavyo vitasaidia vijana wengi Kupata ajira”Kasikana Mmbunifu wa Mavazi  Mkoani Geita.

 

Kasikana ameongeza kuwa  ni vyema kwa Watanzania wakapenda vitu vinavyotengenezwa Nchini ikiwa ni pamoja na kuwatumia wabunifu mbali mbali nguo au vitu ambavyo wanaviitaji na kwamba matarajio ya jukwaa hilo ni kuwafikia wabunifu waliopo Kwenye Wilaya  tano zilizopo Mkoani Geita pamoja na ambao wapo vijijini ambao bado awajapata nafasi ya Kutangaza vitu ambavyo wanabuni.

“Hivyo natangaza rasmi kwamba natarajia Kutambulisha jukwaa hili na kuzindua ifikapo tarehe 3/3/2023  kwenye ukumbi wa Otonde Plaza ndani ya uzinduzi natarajia kuonesha ubunifu wangu na kuwatambulisha baadhi ya wanamitindo ambao watakuwa wamevaa mavazi yaliyobuniwa”Kasikana Mbunifu wa mavazi Mkoa wa Geita


“Pia  kutakuwa na mavazi ambayo yatauzwa hapo hapo. mara bada ya uzinduzi na utambulisho wa jukwaa hili tutaanza mchakato wa maandalizi ya Tamasha kubwa la mitindo ambalo tunatarajia kulifanya mwezi wa12 mwaka huu”Kasikana Mbunifu wa mavazi Mkoa wa Geita.








 

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: