Na Angela Msimbira, OR-TAMISEMI


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewaelekeza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma bara za afya ili kuwahamasisha wananchi kuendelea kujiunga na Mfuko wa  Bima ya Afya  kwa Jamii(CHF).

Kairuki ameyasema hayo leo Februari 22, 2023 jijini Dodoma wakati wa kuufunga mkutano mkuu wa mwaka wa Wanganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri.

Amesema uelimishaji huo uendane sambamba na uboreshaji wa huduma kwa wateja, upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Amesema pamoja na mafanikio ya yaliyopatikana kutokana na matumizi ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF)  ambayo ni ongezeko la michango ya wanachama kutoka Sh bilioni 2.2 kwa mwaka 2018 hadi shilingi bilioni 30.2 kwa mwaka 2022, bado jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu kujiunga na mfuko wa bima ya afya  kwa jamii iliyoboreshwa

Aidha, Kairuki amewaagiza waganga wakuu hao kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma  zinazokusudiwa kwa wananchi.

Amesema uchambuzi wa utekelezaji wa miradi hiyo unaoneshajumla ya miradi 208 sawa na asilimia 14 ipo katika hatua ya chini ya lenta, miradi 106 sawa na asilimia 8 ipo katika hatua ya upauaji na miradi 845 sawa na asilimia 58 ipo katika hatua ya umaliziaji.

“Ninawaagiza miradi iliyopo kwenye upauaji ikamilike ifikapo tarehe Februari 28 mwaka huu na ile iliyopo kwenye lenta iikamilike kabla au ifikapo Machi 31 mwaka huu.”

Waziri Kairuki amesema moja ya kigezo  kitakachotumika kupima utendaji kazi wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri ni ni utekelezaji wa majukumu yao kwa weledi na kuwataka kutimiza wajibu wao wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pia amewataka kuhakikisha wanashirikiana na idara nyingine pamoja na wakaguzi wa ndani  kukagua  bidhaa za  afya na kitakuwa kiashiria  cha ufanisi. 

“ Kutokana na changamoto hii mkasimamie vituo vya kutolea huduma za afya na kuweka bajeti ya ununuzi ya vifaa vyakufanyia tathmini ya lishe kama vile mizani, mbao za kupimia urefu, utepe wa wakupimia mzingo wa mkono na chakula dawa kwenye mipango ya vituo vya kutolea huduma za afya na utekelezaji wake.”

“ Niwasisitize waganga wakuu wa mikoa na halmasahuri kuendelea kusimamia kwa karibu upatikanajiwa taarifa na takwimu kwa makundi haya maalum ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kijamii.”

Aidha, amewataka kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kuimarisha usimamizi kwa njia ya kuhamasisha maadili yautumishi wa umma miongoni mwa watumishi wa afya kwa kuwa kutokuzingatia kwa maadili sio tu kuna-athiri mahusiano baina ya watoa huduma na watumia huduma.

Share To:

Post A Comment: