Na Denis Chambi, Tanga. 

Waziri wa maji Jumaa Aweso ameitaka mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira 'Tanga Uwasa' kutoa taarifa mapema kwa wananchi pale inapotokea changamoto ya kukosekana kwa huduma hiyo ili kuondokana na malalamiko yanayoweza kujiyokeza huku akiiagiza mamlaka ya bonde la mto pangani kufanya ufwatiliaji kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.

Waziri Aweso ametoa magizo hayo mkoani Tanga wakati akikagua hali ya upatikanaji wa maji kufwatia kukosekana huduma hiyo kwa siku nne mfululizo chanzo kikitajwa kuwa ni uchafuzi wa mazingira uliofanywa na wananchi kayika chanzo kikuu cha mto Zigi hali iliyopelekea maji kuwa katika hali ya uchafu usio kawaida na hivyo kuifanya mamalaka hiyo kusitisha huduma kwa wananchi ili kutatua changamoto hiyo.

 "Jukumu la kutoa huduma ya maji safi na salama kwa jiji la Tanga ni la Tanga uwasa kama mamlaka ya maji , tumepata maelezo ni kwa nini wananchi walipata huduma ya maji isiyo ya kawaida baada ya kuona maji katika hali ile waliamua kuzima mitambo kwahiyo kelele za watu kukosa maji yaliyokuwa yanapatikana zilileta taharuki pamoja na changamoto iliyojitokeza watu wa maabara na wataalamu wameweza kuyatibu na sasa hivi yapo katika hali yake na tumepita kwa wananchi baadhi ya nyumba maji yapo" alisema Aweso.

 "Lakini kubwa ninalotaka kulisisitiza inapotokea changamoto kukosekana kwa maji sio jambo baya lazima taatifa zitolewa kwa wakati kutokutoa taarifa kunaleta tahatuki kwa wananchi, lakini Tanga uwasa utoaji wa huduma ya majisafi na salama ni wajibu na majukumu ya mamlaka yeo kwahiyo lazima wajipange kuhakikisha wanatoa huduma ya maji sagi na salama wakati wote , maji hayana mbadala lakini pamoja na kurejea huduma hii lazima iundwe timu maalum ya kupita kila mtaa kuona huduma ya maji inalejea kama kawaida yake nina imani hili jambo haliwezi kutokea tena" 

"Watu wa bonde la mto Pangani moja ya majukumu yenu ni ulindaji na utunzaji wa vyanzo vya maji inakuwaje mtu afanye shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji pangeni timu ianze kukagua katika vyanzo vya maji mwanzo mpaka mwisho na wale wote ambao wanahusika na shughuli za kibinafamu karibu na vyanzo vya maji sheria ipo lazima tukasimamie sheria haiwezekani kuoneana haya haiwezekani shughuli za madini zifanyike kwenye chanzo cha maji wachukuliwe hatua twendeni tukasimamie sheria iendane sambamba na utoaji wa elimu" alisisitiza Waziri Aweso. 

Aidha waziri Aweso ameitaka bodi ya mamlaka hiyo kukaa na kujadili namna watakavyoweza kupambana na kutatua changamoto zinazopelekea kukosekana kwa maji akiitaka pia kufanya kikao cha pamoja na madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwaeleza hali halisi ya utekelezaji wake hii ikilenga hasa kuweka wazi taarifa za kiutendaji zitakazosaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi. 


Akieleza changamoto iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa siku kadhaa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa Geoffrey Hilly alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo uchimbaji wa madini katika chanzo kibwa cha Mto Zigi kinachotegemewa na mamlaka hiyo hali iliyopelekea kuchafuka kwa maji. 

"Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa maji tangu mwezi wa 10 mwaka 2022 changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa umeme katika maeneo yetu ya kuzalisha maji lakini hivi karibuni ikatokea changamoto ya kuchafuka sana kwa maji na imetokana na hali ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo chetu kikubwa cha mto Zigi na hata usafishaji wake ulikuwa ni wa hali ngumu kwahiyo tukazima kwanza maji yasije tuyatibu na tumefanikiwa na hivyo tayari maji yameshaanza kutoka kwa baadhi ya maeneo" 

Hilly Alisema kuwa Mamlaka hiyo ipo mbioni kwaajili ya kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara ambapo wamejipanga kununua mitambo maalumu ya kudhibiti changamoto ya kupungua kwa umeme , kupatikana kwa mradi mkubwa wa kujenga tanki la kuhifadhia maji ambapo hata itakapotokea changamoto ya umeme bado maji yatakuwa yanapatikana kwa uhakika. 

Kwa upande wake mkurugenzi wa bonde la mto Pangani Segure Segure amekiri uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji licha ya jitihada wananzozifanya akiahidi kupokea na kwenda kutekeleza maagizo ya waziri wa Maji Jumaa Aweso. 

"Bonde la Pangani ndio lenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wenzetu wanaochukuwa maji kwenye vyanzo yana kuwa kwenye ubora stahiki sisi kama watu wa bonde la mto Pangani tumezingatia maelekezo ya viongozi wetu na tumeshajipanga kutekeleza na tumekuwa tukitekeleza hatua mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani serikali za wilaya na mikoa hili la leo limetushtua kwamba yawezekana kuna mahala hatujafanya vizuri zaidi" alisema Segure. 

Akizungumza katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameipongeza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa kwa jitihada za haraka ilizozifanya kutatua changamoto ya kuchafuka kwa maji hali iliyoleta taharuki kwa wakazi wa jiji la Tanga kwa siku nne mfululizo huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo. 

"Niwapongeze sana mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa walikosea mahala pa kutoa taatifa mapema za ukosefu wa maji tatizo waliliona wangetuleta yale maji yangetuathiri sana lakini wakayazuia kwanza ili wapate suluhisho la kuyatibu na hatimaye wamefanikiwa" alisema Mzee. 

Akizungumza mmoja wa madiwani wa Jiji la Tanga Salimu Perembo ameishauri mamlaka hiyo kutanua huduma zake kwa upande wa majitaka hii ikienda sambamba na ongezeko la wananchi na makazi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza. 

Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira inazihudumia wilaya za Tanga Pangani pamoja na Muheza ikiwa inazalisha lita zaidi ya 30 za maji kwa siku ambapo sasa inatekeleza mradi unaogharimu shilingi Billion 9.18 ambao mara baada ya kukamilika utaiwezesha Tanga uwasa kuwa na uhakika maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi.
Share To:

Post A Comment: