Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umewajengea uwezo wa kiuchambuzi kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe katika masuala ya Usawa wa Kijinsia pamoja na masuala mengine ya Ukatili wa Kijinsia hasa kujikita katika kusimamia Usawa wa Kijinsia kwenye sera, mipango, afua, na shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba amesema mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo ili wanapojadili Bajeti za Manispaa au Halmashauri waweze kutoka na mapendekezo ya Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia.

Pia amesema kwa kipindi cha zaidi ya miaka 5 sasa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umekuwa ukiwajengea uwezo Vituo vya Taarifa na Maarifa vilivyoko Ilala, juu ya masuala ya Kijinsia ikiwepo kupambana na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia hasa Ukeketaji, ndoa za utotoni na mimba za utotoni unaoendana na mlengo wa Upangaji wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Selemani Bishagazi  amesema ya vituo hivyo vimefanya mapitio ya haraka wa Bajeti ya Halmashauri ya Jiji letu la Dar es salaam kwa mwaka wa fedha 2022/23 ili kuangalia ni kwanamna gani imezingatia usawa wa Kijinsia katika upangaji wa Bajeti hiyo katika tathmini na uchambuzi huu umelenga kuibua taswira ya kimtazamo ili kujenga msimamo wa Vituo iwapo masuala muhimu ya wanajamii kwenye sekta za elimu, maji, afya na kilimo yamebeba uhalisia wa mahitaji ya wanawake, wasichana na vijana kikamilifu kwa kulingana na uhitaji wao wa kijinsi na kijinsia.

Vituo hivyo vya Taarifa na Maarifa vimesema katika ufuatiliaji wa bajeti ngazi ya Mamlaka za serikali za Mitaa wanaangalia utengwaji wa bajeti kwaajili ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na kuondoa kabisa changamoto za ukosefu wa usawa katika kunufaika na rasilimali za umma pia ufuatiliaji huu unachambua kwa kiwango gani rasilimali za umma zinaelekezwa kwenye huduma zinazokidhi mahitaji ya wanawake, wanaume, na vijana kwa mfumo jumuishi.

TGNP kwa kushirikiana na wadau wake imefanikiwa kujenga uwezo kwa Wizara za kisekta, taasisi, wakala wa serikali asasi na mashirika ya kiraia juu ya uandaaji wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia katika kufanya hivyo mafanikio kadhaa yamefikiwa ikiwepo kwa Halmashauri zaidi ya 30 kutenga Bajeti katoka katika Mapato ya ndani kwaajili ya kuboresha miundombinu ya kutolea elimu kama kujenga matundu ya vyoo, vyumba maalum vya kujisitiri, Kununua Taulo za Kike, kujenga mabweni ya wasichana na kujenga shule za mfano za wasichana.

Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe vimetoa mapendekezo ya vipaumbele muhimu kwenye upangaji wa Bajeti yenye mlego wa Usawa wa Kijinsia kwa wadau wa Usawa wa Kijinisa(Bajeti Jumuishi) kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/24 ili kuweza kunufaisha jamii kwa ujumla.

Wamesema kipaumbele cha kwanza ni Viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili mazao yaliyolimwa katika maeneo mbalimbali ya Ilala yanahitaji kuongezewa thamani kama mboga mboga na matunda zinazolimwa katika Eneo la Kituo cha Kilimo la Kinyamwezi litumike pia kama kiwanda cha wananchi cha kuzalisha bidhaa mbalimbali za kilimo na kuzitafutia masoko ndani na nje ya nchi.

Pia katika Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu wamesema bado kuna ombwe kubwa kati ya hali halisi ya Jamii na dhana ya ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia kwamba uchumi unatakiwa kugusa maisha ya watu moja kwa moja hivyo basi tunapendeleza serikali kuwekeza zaidi kwenye Nyanja za uchumi mdogo wa watu hasa katikia uzalishaji na masoko.
Mwezeshaji wa Mafunzo Dei Temba akifungua mafunzo ya uwezo wa kiuchambuzi  wa Bajeti kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe katika masuala ya Usawa wa Kijinsia pamoja na masuala mengine ya Ukatili wa Kijinsia hasa kujikita katika kusimamia Usawa wa Kijinsia kwenye sera, mipango, afya, na shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni, Sada Ramadhani Shifta
akiwasilisha mchanganuo wa Bajeti ya kilimo ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka wa fedha  wa 2022/23 wakati wa mafunzo ya uwezeshwaji wa kiuchambuzi wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe kilichofanyika Kivule
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule Erick Anderson  akiwasilisha mchanganuo wa Bajeti ya Elimu ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka wa fedha wa 2022/23 wakati wa mafunzo ya uwezeshwaji wa kiuchambuzi wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe kilichofanyika Kivule.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule Zahara Mzee akiwasilisha mchanganuo wa Bajeti ya Elimu ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka wa fedha wa 2022/23 wakati wa mafunzo ya uwezeshwaji wa kiuchambuzi wa Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe kilichofanyika Kivule.
Mlezi Kituo cha Taarifa na Maarifa Kipunguni, Selemani Bishagazi (wa kwanza kushoto) akichangia mada kuhusu Bajeti ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka 2022/23 katika masuala ya Usawa wa Kijinsia pamoja na masuala mengine ya Ukatili wa Kijinsia hasa kujikita katika kusimamia Usawa wa Kijinsia kwenye sera, mipango, afya, na shughuli mbalimbali za maendeleo
Diwani viti Maaalum kata ya Majohe, Semeni Mtoka akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi mbalimbali wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kuhusu Bajeti ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka 2022/23 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiuchambuzi  wa Bajeti kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe 
Diwani wa kata ya Kipunguni, Steven Mushi  azungumzia mikakati pamoja na changamoto wanazozipitia Madiwani hasa kwenye kupanga Bajeti zanye mlengo wa Kijinsia wakati wa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiuchambuzi  wa Bajeti kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe.
Baadhi ya Madiwani, Watendaji pamoja na Viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kata za Kipunguni, Kivule, Zingiziwa na Majohe wakiwa kwenye kikao cha kuwajengea uwezo wa kiuchambuzi kwenye Bajeti yenye mlengo wa Kijinsia hasa kwenye Bajeti ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka 2022/23.
Picha ya Pamoja
Share To:

Post A Comment: