Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiwa na viongozi mbalimbali wakigawa miche ya miti kwa taasisi ya jeshi la JKT lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiwa na viongozi mbalimbali wakigawa miche ya miti kwenye moja ya shule zilizopo wilaya ya Mufindi inayolizunguka shamba la miti la Sao Hill.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego wa pili kushoto akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali wakati wa zoezi la ugawaji wa Miche ya miti kwa wananchi, wadau na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Na Fredy Mgunda, Iringa.


WAKALA wa huduma za misitu Tanzania (TFS )kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa limefanikiwa kugawa zaidi ya miche ya miti milioni moja kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kulinda mazingira ya misitu na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa faida ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill,Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Ignas Lupala  alisema kuwa shamba hutenga miche zaidi  ya milioni moja kwa ajili ya kuigawa kwa jamii na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zilizopo Wilayani Mufindi na maeneo jirani ili ipandwe katika maeneo yao kwa ajili ya kuhifadhi mazingira pamoja na kutumika kama chanzo cha kipato baada ya kuivuna na kuuza hata hivyo miche hiyo inayogawiwa kila mwaka  ina thamani ya takribani TZS 300,000,000/=.

Lupala alisema kuwa Jamii ,Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma
yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya binadamu.

Alisema ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai

Lupala alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.

Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.

“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka hifadhi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema

Lupala alisema kuwa upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.

Aidha lupala alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.

Kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego aliwapongeza TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kwa zoezi la ugawaji wa miche kwa wananchi wanaolizunguka shamba kwa kufanya hivyo kunasidia kujenga uhusiano mzuri baina ya Shamba na wananchi.

Dendego alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill lina umuhimu mkubwa kwa kuwa asilimia 15 ya maji yanayoingia katika bwawa la Mwalimu Nyerere yanatoka katika vyanzo vya maji vinavyopatikana katika Shamba hilo la Miti SaoHill hivyo aliwaomba  wanachi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao na kutunza vyanzo vya maji

"Nawapongeza sana TFS kupitia Shamba la  SaoHill kwa zoezi hili mnalolifanya la kuwapatia wananchi miche na nawaomba msiishie hapa kwani miti inachangia katika ukuaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo msisitishe zoezi hili" alisema Dendego

Dendego alisema kuwa Shamba hilo linachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya nchi yetu na hayo ndiyo yanayotumika katika kutatua changamoto nyingi za wananchi hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kushirikiana na uongozi wa Shamba ili  kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa faida ya Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa misitu iliyopo katika Mkoa wa Iringa imekua na  faida kwa wananchi na taifa kwani inasaidia katika upatikanaji wa malighafi za viwanda na mapato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa  wilaya inashirikiana vyema na uongozi wa Shamba la Miti SaoHill wanajua na kutambua mchango wa Shamba hilo katika Halmashauri zilizopo Wilayani Mufindi na Taifa kwa ujumla.

"Shamba la Miti Sao Hill limekua na mchango mkubwa katika wilaya yetu kwani linasaidia upatikanaji wa malighafi za viwandani na kusaidia katika utunzaji wa mazingira yetu hivyo zoezi hili la ugawaji miche kwa wananchi  linasaidia katika kujenga uhusiano bora baina ya wananchi na shamba"alisema Mtambule

Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonufaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.

“kuchukua hatua za ulinzi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuendelea kunufaika na rasilimali zitokanazo na uhifadhi” walisema wadau

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: