Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina akiongea na vikundi vilivyopata mkopo wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kuutumia vizuri mkopo huu kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina akiwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Flaviani Mpanda wakikabidhi mfano wa hundi ya mkopo ambao wamevipatia vikundi 26 vya Halmashauri hiyo


Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya wilaya ya Mufindi imetoa mikopo kwa jumla ya vikundi 26 wenye thamani ya shilingi millioni 305,000,000 kwa ajili kufanya shughuli za kimaendeleo kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mikopo hiyo kwa vikundi hivyo 26, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alisema kuwa wametoa mikopo kwa vikundi 13 vya wanawake, vijana 12 mlemavu mmoja ambavyo kww ujumla vinakamilisha idadi ya wanachama 414 kutoka katika Halmashauri hiyo.

Mgina alisema kuwa vikundi Vya wanawake vimepata jumla ya mikopo ya kiasi cha shilingi millioni 145,000,000, vikundi vya vijana kiasi cha shilingi millioni 145,000,000 na kikundi cha mlemavu shilingi laki 15,000,000 lengo likiwa ni kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.

Alisema kuwa sambamba na hilo waliwakabidhi vikundi vifaa vitakavyosaidia katika uendeshaji wa miradi yao ambavyo ni Toyo na chain kwa vikundi vya Mwangaza kutoka Kijiji cha Ukami, Pikipiki sita kwa kikundi cha vijana cha amani kutoka Kijiji cha Ugesa kata ya Ihalimba na mashine ya kudurufu moja kutoka kikundi cha Way Forward kutoka Kijiji cha Igowole.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alimazia kwa kuvitaka vikundi vyote vilivyopata mkopo kuhakikisha vinarudisha fedha hizo kwa wakati ili kuwawezesha wananchi wengine kukopa mikopo hiyo.

kwa upande wake makamu mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Flaviani Mpanda ameitaja mikopo hiyo kuwa na tijà zaidi Kwa makundi hayo kwani asilimia kubwa imechochea makundi hayo kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuondosha changamoto za kipato zilizokuwa zikiwakabili.

Mpanda alisema amewahimiza waliopata mikopo katika awamu hii kuhakikisha wanaitumianvyema na kurejesha Kwa wakati Ili kutoa fursa Kwa makundi mengine yatakayohitaji mikopo hiyo Huku akipongeza vikundi ambavyo vinaendelea kurejesha mikopo hiyo inayotolewa kupitia mapato ya ndani katika kuchochea ukuajibwa uchuminkwa vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavuShare To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: