Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda akimkabidhi kishikwambi mmoja ya madiwani wa Manispaa hiyo
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda akimkabidhi kishikwambi mmoja ya madiwani wa Manispaa hiyo.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imegawa vishikwambi kwa madiwani na wakuu wa idara kwa lengo la kurahisisha utendaji wa kazi na kuendana na teknolojia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vishikwambi hivyo, Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa baraza la madiwani wa Manispaa hiyo waliazimia kununua vishikwambi na kuachana na matumizi ya taarifa za kwenye makaratasi.

Ngwanda alisema kuwa kununuliwa kwa vishikwambi hivyo kutapunguza matumizi makubwa ya fedha za vikao kwa ajili ya kuchapisha taarifa hizo.

Alisema kuwa jumla ya vishikwambi 30 vimenunuliwa kwa gharama ya shilingi millioni 18 ambapo vishikwambi hivyo vitatumika kwa miaka mingi.

Aliwataka madiwani na wataalam waliopata vishikwambi hivyo kuvitunza kwa kuwa hiyo ni ofisi na hayupo tayari kusikia taarifa kuwa vishikwambi hivyo vimeibiwa.

Ngwanda alisema kuwa kununulia kwa vishikwambi hivyo kutawarahishia utendaji wa kazi wa madiwani na wataalam kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hapa nchini.

Alimalizia kwa kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kufanikisha kwa kununuliwa kwa vishikwambi hivyo.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani na wataalam walisema wanampongeza Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda kwa kusimamia maazimio ya madiwani kwa wakati.


Walisema kuwa kupatikana kwa vishikwambi hivyo kutasaidia kufanya kazi kwa wakati na kutapunguza matumizi makubwa ya fedha za Serikali wakati wa vikao vya madiwani na matukio mengine ambayo yatakuwa yanahitaji kutolewa taarifa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: