Na Joel Maduka Geita. 




Waumini  mbali mbali wa  Dini ya Waadventista Wasabato Nchini wametakiwa kutambua  majira na nyakati  kwa kutenda mambo yaliyo  mema ikiwa ni pamoja na kuwavuta watu kumtambua Mungu  na kuachana na vitendo viovu ambavyo vimeonekana kuendelea kuugubika Mkoa wa Geita.


Hayo yamesemwa na Askofu wa Jimbo la Nyanza ukanda wa Dhahabu wa Kanisa la  waadventista wasabato ,Enoch Sando ,wakati  akizungumza na waumini wa kanisa hilo kwenye uzinduzi wa Mtaa wa Nyankumbu uliopo Mjini Geita.

 Amesema ni vyema kwa waumini  wa dhehebu hilo wakatumia muda wao mwingi kufanya tafakari ya Mungu ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya uovu ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu ambao bado awajamjua Bwana Yesu Kristu.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: