Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiongea na viongozi na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa zoezi la upandaji miti mkoa wa Iringa lililofanyikia wilaya ya Mufindi.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipanda mti wakati uzinduzi wa zoezi la upandaji miti mkoa wa Iringa.
MEYA wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti mkoa wa Iringa lililofanyikia wilaya ya Mufindi.


Na Fredy Mgunda, Iringa.


MKOA wa Iringa umezindua rasmi zoezi la upandaji miti rafiki na maji katika wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

Akizungumza Mara baada ya kupanda miti mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego alisema kuwa mko wa Iringa unapanda miti Kati ya Milioni 30 hadi 35 kila mwaka kwa lengo kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

Dendego alisema kuwa kutokana na utunzaji wa vyanzo vya maji mkoani Iringa kunasaidia kutoa huduma za maji katika mikoa ya jirani kwa ajili kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Alisema kuwa kila nyumba na taasisi za serikali na binafsi kuhakikisha wanapanda miti kwa ajili ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa faida ya Taifa.

Dendego alisema kuwa Wananchi wanatakiwa kutunza mazingira na kupanda miti rafiki na vyanzo vya maji.

Alisema kuwa asilimia 75 ya mapato mkoa wa Iringa yanatokana na mazao ya miti hivyo wananchi wa mkoa wa Iringa wanapaswa kuendelea kupanda na kutunza miti kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wa Iringa.

Dendego alisema kuwa vishoka hawana nafasi katika mkoa wa Iringa kwa kuwa wamekuwa wakiharibu mazingira na kuharibu soko la miti kutoka mkoa wa Iringa kutokana na uvunaji wa miti ikiwa bado midogo.

"Wananchi na wakulima acheni kuvuna miti ikiwa ambayo haijakomaa inaharibu soko la zao la miti la mkoa wa Iringa"alisema Dendego


Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa unaendelea kupambana na majanga ya moto na kuwataka wananchi kuacha tabia kuchoma Moto kwa kuwa kufanya hivyo kunaharibu mazingira.

Lakini pia mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego aliupongeza uongozi wa shamba la miti la Sao Hill kwa kuendelea kupanda miti na kugawa miti kwa wananchi.


Naye mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wilaya ya Iringa watazindua zoezi la upandaji miti tarehe 19/01/2023 kwa lengo la kuendelea kutunza mazingira na kuvilinda vyanzo vya maji wilivyopo wilayani humo.

Moyo alisema kuwa atahakikisha kila diwani anahamasisha wananchi kwenye kata zao zoezi la upandaji miti kama ambayo mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego alivyoagiza.

Alisema kuwa atahakikisha kila shule iliyopo katika wilaya ya Iringa wanapanda miti kwa lengo la kutunza mazingira na vyanzo vya maji.


Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi,George Kavenuke alisema kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya mkoa wa Iringa kwenye kutunza mazingira na vyanzo vya maji katika mkoa wa Iringa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: