Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali ipo Tayari kuupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, hiyo ni baada ya Kubaini Changamoto ambazo Wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo linapokuja suala la Gharama za Matibabu.


Waziri Ummy amebainisha hayo Januari 23, 2023 Jijini Dar es Salaam Kwenye Kikao kazi baina ya Wizara ya Afya na Wahariri wa Vyombo vya habari nchini kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Waziri Ummy amesema mara baada ya Muswada huyo kupitishwa na Wabunge na Kuwa Sheria kamili, Serikali inafikiria Kuifungamanisha Sheria hiyo na Baadhi ya Upatikanaji wa Huduma za Kijamii kama Vile Leseni ya Biashara, Udereva au Kitambulisho cha Taifa.

"Hatutamuacha nyuma Mtanzania yeyote katika huduma ya afya, Nawaomba wananchi anzeni kudunduliza ili mkate bima ya afya, ninataka muamini bima ya afya si kwa wagonjwa pekee hata wazima wanatakiwa kukata bima ya afya" amesema Waziri Ummy.

Kwa Upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ipo haja kwa Wahariri wa vyombo vya habari kuibeba ajenda ya Bima ya Afya kwa Wote, huku akibainisha kuwa itakapopitishwa na Bunge kuwa Sheria kamili italeta faraja na kuwa msaada mkubwa kwa Wananchi ambao wamekuwa wakibeba mzigo wa Kulipia Gharama kubwa za Matibabu.

"Niwaombe ndugu zangu Wahariri wa vyombo vya habari Mliopo hapa, tulibebe Jambo hili ambalo kwa hakika litakuwa na tija kwa Taifa, ninafahamu nguvu ya kalamu zenu kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili" amesema Msigwa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodautus Balile ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wa Wahariri na vyombo vya habari katika kuisukuma ajenda ya Bima ya afya kwa wote kwa Wananchi, akieleza utayari wa Wahariri kujikita kuisaidia Serikali katika kuwaelimisha Wananchi kutambua umuhimu wa Matumizi ya bima ya Afya.
Share To:

Post A Comment: