Serikali ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania, umekabidhi msaada wa mtambo maalum wa kuchujia maji na kuondoa madini hatari ya floraidi, kwa wananchi wa kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua na kukabidhi mradi huo iliyofanyika kijijini hapo, mgeni rasmi na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yashushi Misawa, amesema kuwa serikali ya Japan imefikia hatua hiyo mara baada ya kutambua kiasi kikubwa cha floraidi kwenye maji ya eneo hilo na kkuon madhara wanayoyapata watu wanaotumia maji hayo.

"Tafiti zinaonesha maji ya eneo hili yanamadini ya frolaidi yaliyozidi mm 24 kwa lita, ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu, mtambo huu utaondoa madini hayo na kufikia  mm 0.1 kwa lita kiasi kinachokubalika kimataifa kwa matumizi ya binadamu" Amebainisha Balozi Misawa.

Aidha Balozi huyo ameweka wazi kuwa, uwepo wa mtambo huo, utasaidia kuondoa changamoto kwa watoto wanaozaliwa sasa na kuwataka wananchi hao kuhakikisha wanatumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani kwa kunywa na kupikia.

Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Mwl. James Mchembe, amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini juhudi za serikali ya  Japan kwa watanzanzia, na inaahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki ili kudumisha ushirikiano huo kwa lengo la kutatua changamoto za kijamii nchini.  

Nao viongozi wawakilishi wa wananchi  licha ya kuushukuru ubalozi wa Japan, wamethibitisha kuwepo madhara makubwa kwa watu kutokana na kutumia maji yenye floraidi iliyozidi na kuahidi kuutunza mtambo pamoja na kuhakikisha matumizi sahihi ya maji hayo hususani kwa watoto.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa amebainisha kuwa, mtambo huo ni neema ya kipekee iliyowashukia wananchi wa Lemanda na kuuomba ubalozi huo kuona umuhimu wa kuongeza mtambo ambao utawafikiwa wananchi wa vitongoji vyote vitatu vyenye changamoto kama hiyo.

"Tunashukuru kwa mtambo huu, Mhe. Balozi kama unavyoshuhudia watoto wetu wamepinda miguu na wengine kuwa na vichwa vikubwa, tukuombe mtusaidi kupata mtambo mwingine utakaowasaidia wananchi wa vitongoji vingine viwili vya kijiji hiki".Amesisitiza Mhe. Raymond Lairumbe, Diwani  wa kata ya Oldonyowas

Akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa Lemanda Afisa Mtendaji wa Kata, Lomunyaki Ndiyogi amebainisha uwepo wa changamoto ya watoto walioathitika na madini ya floraidi kushindwa kutembe na kufika shule hivyo kuiomba serikali ya Japan kujenga madarasa ya awali kwenye kitongoji  cha Ngivilati ili watoto hao waweze kusoma ndani ya kitongoji chao.

Mtambo huo wa kuchuja maji  umetengenezwa na chuo kikuu cha Shunshi cha nchini Japan, una uwezo wa kuzalisha Lita 300 kwa saa na kuhudumia jumla ya 60 na watu zaidi ya 400 wa kitongoji cha Lemanda, umegharimu dola za kimarekani 115,000 sawa na shilingi milioni 264 za kitanzania.

Share To:

Post A Comment: