Na Elizabeth Joseph,Arusha.


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF) umeahidi kulipa mafao ya waliokuwa wanachama wao waloikutwa na vyeti bandia ambao wameaga dunia.


Kauli hiyo imetolewa Disemba 2 na Meneja Uhusiano na Elimu kwa wanachana wa Mfuko huo Bw,James Mlowe wakati akiongea na Waandishi wa habari juu ya mafanikio na changamoto za Mfuko huo Mkoani Arusha.


Alisema kuwa ni haki ya malipo ya mafao kwa wanachama  waliofariki ambapo ndugu ama watoto ambao ndio warithi wanatakiwa kufika katika Ofisi za Mfuko huo na kupewa utaratibu wa malipo hayo.


Aidha alibainisha kuwa tayari Mfuko huo uliwalipa wanachama 750 Kati ya wanachama 9700 ambao wapo kwenye orodha ya PSSSF na orodha ya serikali waliokutwa na vyeti bandia ambapo alitaja jumla ya kiasi wanachotakiwa kulipwa wote ni Bilioni 22.22.


"PSSSF bado inatakiwa kulipa wanachama wengine wa vyeti feki 2800 ambao wapo kwenye orodha ya serikali watalipwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 9.3 hivyo jumla ya Bilioni 31.56 zitalipwa kwa wanachama 12,666 na mchakato bado unaendelea kwa wengine ambao bado wanakamilisha taratibu za kujaza fomu"aliongeza Bw,Mlowe.

Share To:

Post A Comment: