Na, Denis Chambi, Tanga. 

Bondia wa ngumi za kulipwa nyota wa Tanzania Hassan December 30, 2022 atapanda ulingoni kuzichapa na bondia raia wa Marekani Peter Dobson katika pambano lao la kuwania mkanda wa WBC international Super Welter (Vacant) ambao ni kwa mara ya kwanza kugombaniwa nchini Tanzania na Afrika.
Pambano hilo litapigwa Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru 1961 ngumi za kulipwa kuchezwa mara baada ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kuruhusu ngumi za kulipwa visiwani humo, pambano hilo likidhaminiwa na Shomari Kimbau (Golden Boy Africa Promotion).

 Siku hiyo Mwakinyo mwenye miaka 27 atakuwa na kazi ya ziada ya kufanya ili kuwafurahisha watanzania kwani mpinzani wake anayepigana mwenye miaka 32 hajawahi kupoteza hata pambano moja kati ya 16 aliyocheza huku yeye mwenyewe akicheza mapambano 20 na kupoteza matatu mpaka sasa. 

Akizungumza promoto wa pambano hilo Shomari Kimbau alisema kuwa mkanda huo utakaowaniwa siku hiyo utakuwa ni mara ya kwanza kwa Africa na Tanzania ambapo kama Mwakinyo atashinda kanda huo utampandisha mpaka nafasi ya kumi kwa mabondia  10 bora duniani kwenye uzito wake. 

"Pambano hilo litakuwa ni la kihistoria kwa Tanzania na Africa kwa mkanda wa WBC silver international , katika mikanda ambayo ina hadhi na inatambulika duniani huu utakuwa ni mkanda wa kwanza kuja kugombaniwa dunia imekubali kumpa Mwakinyo  hiyo nafasi".alisema Kimbau.

"Mara nyingi tumekuwa tukipata changamoto kwamba mabondia wetu wanashindwa kucheza na mabondia wenye viwango vikubwa duniani kuja kucheza Tanzania , lakini mara hii tumepata hii bahati na iwapo Mwakinyo atashinda itakuwa ni ushindi ambao utamuweka katika nafasi 10 za mabondia  bora duniani na hiyo itampa nafasi zaidi ya kuweza kucheza  hata na  bingwa wa dunia"

 "Kwa upande wangu Promota sina wasiwasi yani asilimia mia namwamini Hassan Mwakinyo ni mtu ambaye anaonekana unapompa jukumu analitekeleza kwa ufanisi  mkubwa tuna uhakika kabisa kwamba mkanda huu utabaki Tanzania" alisema Promota huyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari bondia Hassan Mwakinyo amesema kuwa siku hiyo anakwenda kuwapa burudani watanzania hususani wapenzi na mashabiki wa ngumi hapa nchini na Afrika kwa ujumla licha ya kukiri kuwa hajawahi kuona pambano la mpinzani wake alilopoteza lakini siku hiyo anakwenda kumchafulia rekodi yake kwenye rada za ngumi. 

"Nimejiandaa vizuri ninaamini watanzania wana imani na mimi ziku hizo zitapigwa ngumi zisizo za kawaida yani tutapigana, sijawahi kuona pambano la mpinzani wangu na ni boxer ambaye hajapoteza pambano lolote mpaka sasa pambano letu ndio litakuwa la mara ya kwanza kwake kupoteza ambalo litaonyesha udhaifu wake ni upi lakini kwa sababu maandalizi ni sehemu ya maisha yangu niwahakikishie watanzania kuwa nimejiandaa vizuri" alisema Mwakinyo.

 "Kila mtu anajua unyama wangu ni nini katika ngumi niwaambie kuwa mwenye ngumi zake amerudi mjini na nafikiri Taifa litasimama siku hiyo" aliongeza.


Promota wa ngumi za kulipwa Shomari Kimbau akizungumza na waandishi wa habari kuelekea pambano la bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Peter Dobson litakalopigwa December 30 ,2022 visiwani Zanzibar.

Share To:

Post A Comment: