Na Elizabeth Joseph,Monduli.

KATIKA kuendeleza juhudi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Elimu nchini Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imekabidhi Madarasa mapya 36 ya Elimu ya Sekondari yenye thamani ya shilingi Milioni 720 kwa serikali ya Wilaya ya Monduli.

Akiongea wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Engutoto Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh,Frank Mwaisumbe alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizo na kusema uwepo wa madarasa hayo utasaidia wanafunzi kukaa vizuri na kwa nafasi darasani bila kubanana na hivyo kuongeza ufaulu katika masomo yao.

"Monduli mwaka jana kabla hatujapata fedha za UVICO watoto darasani walikuwa wanakaa 80 hadi 90 ndani ya Darasa moja,leo watoto wanakaa 45 hadi 50 hili ni jambo la kupongezwa na kujivunia kwakuwa tunaongeza ufaulu kwa watoto hawa"alisema Mwaisumbe.

Mh,Mwaisumbe pia aliwakata wale wote wanaobeza maendeleo yanayofanywa na serikali ya Rais Samia kwa kusema inakopa sana fedha kuacha mara moja kwakuwa Tanzania bado inahitaji kupiga hatua katika maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu.

"Kuna watu wanabeza kwamba nchi yetu tunakopa sana,kukopa maana yake una vipaumbele vinavyohitaji kutimizwa kwa wakati huu ili ujijenge kwa wakati ujao usiweze kukopa lakini vilevile wakati ni ukuta tukisema tusubiri tozo na fedha tunazokusanya kwenye Kodi hawa watoto watakuwa na miaka 15 wakati wanatakiwa kuanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 7"alisisitiza Mh, Mwaisumbe.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mh,Raphael Siumbu akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo alibainisha kuwa ujenzi wa madarasa hayo ulianza rasmi Oktoba mwaka huu na kukamilika Disemba 3 2022 hivyo kumpongeza Rais Samia kwa fedha hizo.

"Tumefanikiwa kuweka viti na meza 50 kwa kila darasa na kufanya jumla ya viti na meza kuwa 1800 kwa madarasa yote 36,Monduli tulikuwa na upungufu wa madarasa 36 ambayo ilipaswa yajengwe na wananchi hivyo Mheshiwa Rais ametusaidia sana katika hilo na anastahili kupongezwa"alisisitiza Siumbu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh,Isack Copriano licha ya kutoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia aliwashukuru Wakuu wa Shule za Sekondari wilayani humo kwa kwa ushirikiano walioutoa kwa Halmashauri hiyo katika kutekeleza ujenzi wa madarasa hayo.

Share To:

Post A Comment: