Mtendaji mkuu na mkurugenzi wa benchi la ufundi la timu ya Misitu FC Kamote Francis akimpongeza mchezaji wa timu hiyo mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya fainali kweye michuano ya ligi ya mkoa wa Tanga 'TRFA' baada ya kuwafunga Veterans Middle Age goli 1-0 katika uwanja wa CCM Mkwakwani jana jumatano.

Denis Chambi, Tanga. 

SAFARI  ya mabingwa watetezi wa ligi ya mkoa wa Tanga' TRFA Cup' wa msimu uliopita timu ya Veterans Middle Age kulisaka kombe hilo msimu huu juzi jumatano ilifika ukingoni baada ya kukubali kuchapo cha goli 1-0 mbele ya Misitu FC walipokutana katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga kwenye mchezo wao wa nusu fainali. 

Mchezo mwingine nusu fainali ya kwanza uliowakutanisha Eagle Rangers dhidi ya Watumishi FC siku ya jumaane ulishudiwa ukiamuliwa kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu zote mbili kumaliza dakika 90 za mchezo wakifungana 1- 1 ambapo Eagle Rangers kuibuka kidedea. 

Mtendaji mkuu na mkurugenzi wa benchi la ufundi la timu ya Misitu FC Kamote Francis alisema mpaka sasa tayari wamejipanga kwenda kuuwakilisha mkoa wa Tanga kwenye michuano ya mabingwa wa mikoa RCL ambayo itakuwa ni safari yao ya kuelekea lihi daraja la pili msimj ujao.

 Alisema ni furaha kwao kwenda kucheza fainali za ligi ya mkoa ikiwa ni hatua ya kipekee kuiwakilisha wilaya ya Lushoto ambayo haijawahi kuutwaa ubingwa huo ambapo aliwahakikishia mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuubeba ubingwa wa mkoa msimu huu. 

"Ni furaha kwetu kuingia fainali ni jambo la msingi na maendeleo katika soka na mpaka hapa tulupofikia sisi tunataka tuwe mabingwa wa mkoa hivyo tunaendelea kujipanga kuhakikisha tunatimiza lengo letu lakini kubwa tunataka tusogee mbele Zaidi ya hapa tulipo " 

Kamote aliongeza kuwa kwa namna mkoa wa Tanga ulivyokuwa na maendeleo katika sekta ya michezo inashangaza mpaka sasa kuona bado unawakilishwa na timu moja ya ligi kuu ambayo ni Coastal Union 'Wagosi wa kaya' akitamani kuona zaidi ya timu nne zipo kwenye madaraja yote ya michuano ya mpira wa miguu hapa nchini. 

"Sisi hatuangalii wilaya ya Lushoto peke yake maana tumeshavuka huko lakini tunachokiangalia sasa hivi ni kuja kuiwakilisha Tanga kwa ngazi ya kanda ya kaskazini , mkoa wa Tanga kuwa na timu moja ya ligi kuu bado ni changamoto kwa sababu kuna vipaji vingi sana mitaani lakini jinsi ya kuvionyesha ni kutafuta nafasi ya kupata timu nyingine ya ligi kuu angalau tukiwa na timu nne ndani ya mkoa wa Tanga zinazoshiriki ligi kuu vipaji vilivyopo vitaonekana zaidi" alisema. 

Fainali za ligi hiyo ya mkoa zitacheza january 4, 2023 katika uwanja wa CCM Mkwakwani kwa Misitu FC kuvaana na Eagle Ranger kumtafuta bingwa wa msimu huu ambapo kama Misitu akichukua taji hilo atakuwa ameandika historia ya kipekee kwa wilaya ya Lushoto kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa wa mkoa wa Tanga.. 
Share To:

Post A Comment: