Na Mario Mgimba 

Njombe


Kutokana na kauli aliyoitoa baada ya kutoridhishwa na mwenedo  Mradi wa Maji  Igando -Kijombe wenye dhamni ya zaidi ya  bilioni 10 Mhandisi Clement Kivegalo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji  Safi na Usafi wa mazingira Vijijini RUWASA  Nchini ameipongeza kampuni ya  STC Contruction Ltd kwakutekeleza mapungufu yaliyo jitokeza.


Akizungumza mara baada ya kutembeleaa mradi huo wa maji Igando -Kijombe ameweza kuridhishwa na ujenzi ambao unaendelea kutokana na marekebisho ambayo amefanyika kwa sehemu ambazo zilikuwa na changamoto kurekebishwa.


''Sikufurahishwa katika maeneo mawili ambayo ni mwenendo wa kazi unavo enda na kazi zilizokuwa zimefanyika naamini kwakile niliho kiona  ndani ya muda mfupi Watanzania wataanza kunufaika na matunda ya serkali ya awamu ya sita''Alisema Mkurugenzi RUWASA Clement Kivegalo


Aidha akiendelea kuzungumza na wakandarasi wa mradi huo  Kivegalo akaweka bayana namna Mamlaka ya Maji ilivojipanga kutoa huduma bora za maji  kwa wananchi huku akisisitiza taratibu ambazo wamekuwa wakizitoa kwa wale ambao wanajaribu kufanya kazi kinyume na matarajio ya serikali  inavotaka wakati mradi ukiwa  unatekelezwa.


''Tukishatoa Maagizo yakutoridhishwa utekelezwaji wa mradi nilazima wafuate marekebisho ya sehemu ambazo zimeonesha changamoto tulizo waambia,  utakuta Mkandarasi anadai malipo wakati utekelezaji wenyewe hauridhishwi nikushukuru Mkurugenzi  kufanya maboresho niliyokwamba na kufikia hatua ya mwisho katika kazi''Alisema Mkurugenzi RUWASA Clement Kivegalo


Agastine Kwai Mhandisi wa Mradi wa Maji wa Malangali-Njawano alisema kutokana na mapungufu yaliyo kuwa yamejitokeza kwenye maeneo mbalimbali ya mradi yamweweza fanyiwa marekebisho kwa kuendelea na utendaji kazi ambapo  timu ya watalaamu  imeweza kuongezwa ili kuboresha maeneo ambayo yamebaki ilikukamilika kwa mradi huo.


Nae Mhadisi wa RUWASA Wilaya ya  Wangingombe Charse Mengo alisema zaidia ya watu elfu kumi na nne badaa ya kukamilika kwa mradi huo wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji  ambapo tayari  vijiji vya  Malangali na  Njawanu wameanza kupata maji.


Frola Kweya na Frenk Sanga wakazi wa kijiji cha Kangama wilaya Mbalali wananchi watakao nufaika na mradi huo wameishukuru serikali kwa kuweza kuboresha miundombinu rafiki ya maji ambayo itaenda kupunguza changamoto ya majiiliyokuwa ikiwa kabili.

Share To:

Post A Comment: