Na John Walter-Babati

Katika kusheherekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwake, Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imefanya Bonanza la michezo mbalimbali  iliyohusisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.

 

Akizungumzia bonanza hilo mkurugenzi mtendaji David Mulokozi,  amesema dhumuni la michezo hiyo ni  kuboresha afya zao na kujenga umoja kwa wafanyakazi pamoja na sherehe za kutimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka 2018 ambayo  makao makuu yake ni mjini Babati mkoani wa Manyara.

 

Mulokozi amesema Kampuni ya Mati Super Brands inajivunia kukua na kuajiri watu zaidi ya ya 250 kutoka watu watatu walioajiriwa kampuni ikianza.

 

Ameeleza kuwa, Kupitia ajira hizo wamegusa maisha ya Watanzania wengi ambao wameweza kuendesha familia zao, kujenga na hata kusomesha.

 

Mulokozi amesema kilele cha sherehe hizo zitahitimishwa Desemba 31,2022.

 

Mati super Brands Ltd ni wazalishaji na wasambazaji wa Vinywaji vya Strong Dry Gin, Sed Pinneaple Flavour Gin, Tanzanite na Strong Coffee.

Share To:

Post A Comment: