Na Elizabeth Joseph, Monduli.


Katika kuelekea maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara watanzania wametakiwa kuwaenzi Waasisi wa Taifa kwa kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu na Miundombinu.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Monduli Bw Robert Siyantemi wakati wa Kongamano la Miaka 61 ya Uhuru lililohusisha mdahalo kwa wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii na Shule za Sekondari Monduli.


Siyantemi alisema kuwa kila awamu ya Uongozi wa Tanzania umefanya kazi kubwa kuwa kulinda umoja na amani jambo alilosema limechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo.


"Wataanzania tuenzi na kuendeleleza juhudi za viongozi wetu za kuitoa Tanzania katika ulimwengu wa dunia ya tatu na kuipeleka kwenye ulimwengu wa dunia ya kwanza,kila mmoja anapaswa kujiuliza analifanyia nini taifa letu katika kuliinua kiuchumi na maendeleo zaidi"aliongeza kusema Siyantemi.


Naye Alkado Makukuru ambaye ni mwanachuo alishukuru kwa kongamano hilo na kusema limewakumbusha wapi wametoka na wapi walipo na kuipongeza serikali kwa jitihada kubwa inayofanya kuleta maendeleo nchini.


Wilaya ya Monduli itaadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara Disemba 9 katika viwanja vya Barafu Mto wa Mbu ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Mh,Frank Mwaisumbe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Share To:

Post A Comment: