Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kuendelea kuboresha viwanja vya michezo mbalimbali jijini Dodoma ili kuvifanya kuwa rafiki na kusaidia kukuza vipaji.


Mbunge Mavunde kayasema hayo juzi Hombolo Bwawani,wakati akihitimisha fainali za mashindano ya Mavunde CUP Hombolo 2022 ambapo zaidi ya Timu 32 kutoka maeneo mbalimbali zilishiriki.

“Nawapongeza washiriki wote na washindi wa mashindano haya ya mwaka 2022.

Tutaendelea kuyaboresha mashindano haya kila mwaka ili iwe sehemu sahihi ya kukuza na kuvilea vipaji vya wachezaji wengi wa Dodoma.

Lakini pia nitahakikisha naendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya kuchezea michezo mbalimbali hapa Jijini Dodoma ili vijana wengi zaidi wapate fursa ya kuinua na kuendeleza vipaji vyao.

Kwa sasa nachonga viwanja na kuweka magoli ya chuma katika maeneo mengi sana hapa Jijini Dodoma kwa lengo la kuwa na maeneo mengi ya michezo.Na hichi kiwanja cha Hombolo tutakiboresha ili kiwe rafiki kwa ajili ya michezo”Alisema Mavunde

Akizungumza awali,Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Mh Assedi Ndajilo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuandaa mashindano hayo kwa kata ya Hombolo kwa mwaka wa 10 mfululizo,mashindano ambayo yameibua vijana wengi kupata Timu za madaraja ya juu nchini.

Katika mashindano hayo timu ya Red Scorpion ya Hombolo Makulu iliibuka Mabingwa kwa kuifunga timu ya Mwenge FC ya Mkoyo kwa  mabao 3-0 na kujinyakulia kitita cha Tsh 1,000,000,kombe na medali.Share To:

Post A Comment: