Na mario mgimba, Njombe

Wakati Tanzania ikiendelea kupinga ukatili wa kijinsia kupitia siku 16 za kukabilibiana na janga hilo Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema hata vitendo vinavyofanywa na wanaume kwa wanafunzi mbalimbali vyuoni ikiwemo kuwanunulia simu,gari na hata kuwapangishia nyumba ni ukatili unaopaswa kupigwa vita.Kissa ameeleza hayo katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika WILDAF unaofadhiliwa na shirika la kimarekani la maendeleo kimataifa USAIDS uliofanyika mkoani Njombe ukihusisha wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati takribani sita."Mnaposoma wapo wengine wananunuliwa vigali aina ya IST,wapo wengine wanapangishiwa nyumba kubwa,huu nao ni ukatili Kwasababu mwisho wa siku wanakunyima fursa ya kwenda kumiliki vya kwako"amesema Kissa KasongwaVile vile amesema yeye binafsi kungekuwa na uwezekano angeshauri wazazi wasiweze kuwapeleka watoto shule za bweni wakiwa na umri mdogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakikabiliwa na ukatili mkubwa huku akipendekeza angalau watoto waanze wakiwa kidato cha kwanza na kama kukiwa na ulazima kwenda shule za bweni katika umri mdogo basi ziwekwe sheria na miongozo ambayo itaziangalia shule hizo.

Share To:

Post A Comment: