Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Angellah Kairuki ameagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ,Muhandisi wa Halmashauri ya Arusha pamoja na mkaguzi wa ndani ya Halmashauri hiyo kuwasilisha ripoti katika Ofisi yake ndani ya siku saba ili kujiridhisha gharama halisi ya mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kiutu iliyopo katika Halmashauri ya Arusha.


Hatua hiyo imefuatia baada ya taarifa ya mradi wa shule ya sekondari ya Kata Kiutu kutoka kwa  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Suleman Msumi kukinzana na ya Mhandisi wa halmashauri Nuru Mkwazu.



Akitoa maelekezo hayo katika ziara yake mkoani Arusha baada ya kutembelea mradi huo,Waziri Kairuki amesema  uchunguzi ufanyike kwa kina kupitia  idara hizo kwa muda  na ifikapo Desemba 24 ripoti kamili iwe imeshamfikia

 

Akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa shule ya kata ya kiutu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Suleman Msumi amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulitarajiwa kughalimu kiasi Cha sh milion miasita tisini na sita na laki mbili kiasi kilichotumika ni milioni mianne sabini fedha zilizotolewa na Serikali kwa awamu ya kwanza lakini kutokana na maelezo ya Mhandisi wa Halmashauri mradi huo ulitarajiwa kughalimu kiasi Cha shilingi milioni mianane ishirini na sita.

Share To:

Post A Comment: