Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema mpaka sasa idadi ya waliofariki katika ajali ya Ndege ya Precision Air wamefikia 19 huku akisisitiza kuwa kwa namna ndege hiyo ilivyotumbukia katika ziwa Victoria kwa kutangulizi kichwa hakuna matumaini ya rubani wa ndege hiyo kuwa hai.


Waziri mkuu amesema hayo akiwa katika eneo la ajali baada ya kuwasili mchana wa leo na kuongeza kuwa zoezi linaloendelea na kwa sasa kinachoendelea ni utambuzi wa watu waliopoteza maisha na kufanya utaratibu wa kuwapata ndugu zao.
Share To:

Post A Comment: