Kikao cha Kamati ya Lishe wilayani Serengeti kimewataka watendaji wa kata na vijiji kusimamia kikamilifu afua za lishe   mashuleni kwa kushirikiana na  kamati za  shule na kuhamasisha wazazi na walezi kupitia vikao na mikutano mbalimbali.

Hayo yameazimiwa katika kikao cha robo ya kwanza cha lishe kilichofanyika  katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti,akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kamati ya Lishe ambae ni pia  Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  Ndg Kivuma H. Msangi amesema  katika tathimini iliyofanyika ya programu ya  utoaji wa huduma za chakula na  lishe mashuleni wilaya ya Serengeti ina  asilimia 29.61,ambapo  kati ya shule 179 ni 53 zinatoa chakula  kwa wanafunzi shuleni  hivyo ikionesha eneo ilo wilaya haifanyi vizuri.

Ameongeza pia katika  kuhakikisha wanafunzi   wanapata utulivu wa akili na afya ni muhimu watendaji wa kata na vijiji kwa kushirikiana na viongozi wote wakiwemo wa shule wanalivalia njuga   swala la lishe mashuleni ili utendaji wa wilaya uwe kwa asilimia 100 kwenye eneo hilo.

Nae Mganga Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Emiliana Donald amewashukuru viongozi  na shule ambao wamelipa kipaumbele swala hilo la lishe na kuwaomba kuibeba ajenda hiyo ya lishe kwenye  mikutano ya hadhari na maeneo mbalimbali.

Kamati   imewasisitiza wazazi kuwa mstari wa mbele katika swala la lishe na chakula   kwa ajili ya watoto wao wawapo shuleni na kuitaka kila shule kuandaa mpango kazi wa lishe na chakula  na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu.

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imeendelea kujizatiti na kuongeza juhudi katika kuimarisha afua mbalimbali za Lishe ambapo katika tathimi ya Robo ya Kwanza ‘’score card’’

Katika upande wa  ziara za usimamizi  vituoni kuhusu masuala ya lishe 100%,watoto waliopata walipatiwa nyongeza ya matone ya vitamini A  Jumla ya watoto 70948 kati ya watoto 70677 sawa na 100%, 

Jumla ya akina mama/Walezi 36,325 kati ya  36,760 walipatiwa elimu ya Afya kutoka kwa watoa huduma za Afya sawa na 98.8%, Jumla ya mitaa na vijiji 72 viliazimisha siku ya afya na lishe kati ya 101 sawa na 71.3%, Jumla ya akina mama/Walezi 20,071 kati ya 8,645 walipatiwa elimu ya Afya ngazi ya jamii sawa na zaidi ya asilimia 100, 

Utoaji wa dawa za kuongeza damu (IFA) kwa akina mama wajawazito umefanyika kwa 91.4%. Kina mama 14,589 wamepatiwa dawa za kuongeza damu kati ya 15,967.Aidha Wilaya itaendelea  kuongeza juhudi wenye utekelezaji wa shughuli za lishe.
Share To:

Post A Comment: